HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 4, 2024

Waziri Mkuu Majaliwa azindua kituo cha Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Nyang’wale Mkoani Geita

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyang’wale Mkoani Geita, ambacho ni cha Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Sera, Bunge na Uratibu, Bi. Ummy Nderiananga, wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa baraza hilo, Profeesa Aurelia Kamuzora, wa kwanza kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Bw.Nicholaus Kasendawila, wa pili kulia Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale, Bi. Grace Kingalame na watatu kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyang’wale, Bw. Hussein Kassu picha na mwandishi wetu Nyang’wale Geita.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mjasiriamali Mwalimu Reheme Mwakalanga anayetengeneza nguo za batiki wakati alipotembelea mabanda ya wajasiriamali mara baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyangw’ale Mkoani Geita ambacho ni cha Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wa pili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Aurelia Kamuzora, kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela. Picha na mwandishi wetu Nyang’wale Geita.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mjasiriamali Mwalimu Agnes Boniface ambaye anasindika mazao ya alizeti kupata mafuta ya kupikia na mazao mengine kupata viungo mbalimbali mara baada ya kuzindua jenggo la Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyang’wale Mkoani Geita ambacho ni kituo cha Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, B. Beng’i Issa na kulia nia Mwnyekiti wa Baraza hilo, Profesa Aurelia Kamuzora na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Bw. Martin Shigela. Picha na mwandishi wetu, Nyang’wale Geita.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua jiwe la Msingi katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Nyang’wale kuwa kitu hicho kimezinduliwa, kituo hicho ni cha Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Isssa,kulia ambaye haonekani vizuri ni mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela na wapili kutoka kulia ni Naibu Waziri Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga. Picha na Mwandishi wetu, Nyang’wale Geita.


WANANCHI wa Wilaya ya Nywang’wale Mkoani Geita wametakiwa kukitumia Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichojengwa wilayani kwao kuanzisha shughuli za biashara na ujasiriamali ili kuwasaidia kuwa na vipato na kushiriki katika Uchumi wa taifa lao

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipokuwa akizindua Kituo hicho ambacho ni kituo cha Baraza la Uwezeshaji Wananchi (NEEC), ambacho kitafanya kazi ya kuwasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali za uwezeshaji kushiriki katika Uchumi wa nchi.

“Wilaya hii imejaliwa kuwa na fursa nyingi ikiwemo ya kilimo, ufugaji, madini hivyo kituo hiki kimejengwa kwa nia ya kuwaletea huduma karibu,” huduma zitakazotolewa ni Pamoja na elimu ya ujasiriamali, urasimishaji wa biashara na kupata mikopo nafuu, alifafanua.

Alisema kwa sasa hakunasababu ya wananchi kulalamikia mitaji kwa vile serikali imewaletea jengo hilo na mikopo itapatikana hapo na kwenye halmashauri bali wao kuchangamkia fursa hiyo.

Hatahivyo asisitiza kwamba wakifanikiwa kupata mikopo hiyo inayotolewa katika jengo hilo wanahitajika kurudisha ili na wengine waweze kukopa.

Alisema wananchi wakope na waanzishe viwanda mbalimbali vidogovidogo vya kusindika mazao, chelehani kushona nguo, kutengeneza batiki, na wafanyakazi waende wakakope wajenge makadhi yao bora.

Alitaja shughuli fursa nyingine zilizopo mkoani humo ni Pamoja na uvuvi, na aliwataka kubadilika kuacha kufuga ngo’mbe kwa mazoe bali wafuge kisasa wawe wachache lakini wenye tija.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema kituo hicho kitasaidia kuwavutia wananchi kufanya shughuli za biashara na ujasiriamali kwa vile ndani ya jengo hilo kutakuwa na taasisi mbalimbali za kuwasaidia kuwapa huduma kwa haraka na kwa karibu kutimiza ndoto zao.

“Katika jengo hili kutakuwa waratibu wa wilaya na mikoa wa baraza, na taasisi nyingine kama benki ya NMB, CRDB, SIDO, TRA, BRELA, TANTRADE, NIDA, TBS na Mfuko wa Self Microfinance,” alisema, Bi. Beng’i

Aliongeza kusema kwamba kituo hicho kinafanya baraza sasa kuwa na vituo 20 nchi nzima na vinge vinaendelea kujengwa na tayari vituo hivyo vimeeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.

Vilevile alisema hadi sasa watu 21852 wamesha tembelea vituo hivyo na biashara zimesha rasimishwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema mafanikio yanayopatikana katika mkoa huo yanatokana na mshikamano ambao wameujenga na hiyo imekuwa ni nyenzo katika utendaji na utoaji huduma bora kwa wananchi.

“Tutahakikisha tunafanya kazi ya kusawasaidi awananchi wetu kulitumia jengo hilo,” dhamira yetu watu waweze kuwa matajiri kupitia shughuli za biashara na ujasiriamali, aliongeza kusema.

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo la kituo hicho pia Waziri Mkuu alifanya Mkutano na wananchi wa wilaya hiyo na kuzindua mwongozo wa Uratibu wa Uanzishaji na Usimamizi wa Vituo vya Uwezeshaji ili kuwezesha wananchi kushiriki katika Uchumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad