HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 11, 2024

GAWIO LA BILIONI 12.2 LIMETOLEWA NA KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA ENERGY TANZANIA KWA RAIS SAMIA

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imempongeza Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira Mazuri ya uwekezaji ambayo yamesababisha kuweza kukabidhi gawio la Sh.Bilioni 12.2 kwa Serikali na kuahidi kuendelea kuboresha huduma zao ili kufanya vizuri zaidi.

Gawio hilo wamelikabidhi leo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia na kwa leo amepokea gawio kutoka kwa Kampuni 10 ambazo Serikali inahisa zake na Kampuni hiyo ni miongoni mwa Kampuni hizo.

Akizungumza baada ya kukabidhi gawio, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah amesema wanaushukuru Rais Samia ambaye ndio jemedari wetu wa kiuchumi nchini Tanzania.

"Ameweza kutoongoza vizuri, ameweka mazingira wezeshi kwa sisi wawekezaji kufanya biashara kwa usalama na ubunifu .Pia tunatoa shukrani kwa Wizara ya Nishati chini Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Dotto Biteko wamekuwa ni viongozi ambao wamekuwa wakituelekeza na kutushauri lakini wamekuwa wakiweka mazingira yanayotuwezesha kufanya kazi vizuri .

"Pia tunamshukuru Msajili wa Hazina ambaye amekuwa kiungo muhimu kwetu sisi kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri na hatimaye tumetoa gawio leo la

sh.bilioni 12.2 .Kigezo kikubwa ambacho kimewazesha kutoa gawio hilo kinatokana na kufanya kazi vizuri Bodi yetu chini ya Mwenyekiti Dk . Selemani Majige ambao ambao wamekuwa wakituelekeza na kutupa ushauri mzuri,"amesema Fatma Abdallah.

Akieleza zaidi amesema katika kuendeleza ufanisi kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma na kuziboresha na kwamba mikakati yao ni kutoa huduma kidigitali katika kutoa huduma zao na mwaka huu wamepanga uwafikia watanzania wengi kwenye kusambaza nishati.

Pia amesema wameona Serikali ilivyoweka nguvu katika nishati safi hivyo na wao wameamua kuweka nguvu katika kufanikisha malengo ya Serikali katika eneo la Nishati Safi ya kupikia kama ilivyo dhamira ya Rais Dk Samia ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi.

Pia amesema Wana mpango wa kuzindua kituo cha gesi kwa ajilli ya kujaza katika magari na uzinduzi huo wanatarajia kuufanya mwaka huu huku akisisitiza wanajivunia kutoa gawio hilo kwani kumekuwa na ongezeko kubwa kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.


 

 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan(katikati) akipokea gawio la Sh.Bilioni 12.2 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Fatma Abdallah (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Dk.Seleman Majige(kushoto). Gawio hilo limekabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudia na wakuu wa taasisi na mashirika mbalimbali ambayo yamehudhuria tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad