HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 12, 2024

DOYO HASSAN DOYO ACHUKUA FOMU UENYEKITI ADC

 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Innocent Siriwa (kushoto) akimkabidhi fomu ya kugombea Uenyekiti Taifa, Doyo Hassani Doyo, leo Juni 11, 2024 katika Makao Makuu ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Buguruni Ilala Dar es Salaam.


Mgombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Bara, Scola Stika Kahana,  akionyesha fomu yake.


Na Mwandishi Wetu 
KATIBU wa Cchama Cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo, leo Juni 11, 20 amechukua fomu kuwania uenyekiti wa chama hicho huku akiahidi mambo mbali mbali ikiwemo kusukuma ajenda za mabadiliko kwenye sheria zilizo na shida.

Doyo ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa chama hicho kinachaoongozwa na Mwenyekiti wake, Hamad Rashid ambaye anamaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya chama hicho amechukua fomu huku akkiahidi kuimarisha chama hicho katika kanda zote nchini, jambo linalotarajiwa kuongeza ushawishi na nguvu ya ADC katika medani ya Siasa ya Tanzania.

Hafla ya uchukuaji fomu imefanyika kwenye Makao Makuu ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Buguruni Ilala Dar es Salaam ambapo pia mgombea nafasi ya Makamo Mwenyekiti Bara, Scola Stika Kahana alichukua fomu.

Doyo pia aliongozana na baadhi ya Wanachama wanaomuunga mkono, akiwemo Mwenyekiti wa Vijana Taifa, Pogora Ibrahimu Pogora na Mwenyekiti wa Kinamama Taifa, Zuwena Mohamed Abdallah kurejesha fomu ya kuwania Fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu, Doyo amesema kuwa akipata ridhaa ya kuwa Mwenyekiti wa chama hicho atasukuma ajenda za kupeleka mabadiliko kwenye sheria alizosema zina matatizo ahadi aliyoizungumza tangu siku alipotangaza nia.

"Nitaenda Kwenye majukumu ya kisiasa kusukuma ajenda za kuleta mabadiliko ya kisheria kwa zile zenye matatizo na pia kusukuma ajenda bora kwa Watanzaniai.

Amesema, maisha ni magumu ili kujikwamua kunahitajika msukumo wa viongozi kama mimi ili Serikali iliyopo madarakani ione namna ya kufanya marejeo ya sera zake, amesema.

Aidha ameongeza kuwa atafanya siasa safi na za kistaarabu kwa mikakati ya kuijenga ADC ili kiwe chama mbadala kitakachoshida katika uchaguzi wa serikali za mitaaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Katiba ya ADC inasema nafasi ya kiongozi ni vipindi viwili vya miaka 5 kila kimoja na baada ya hapo mtu huyo hatoruhusiwa kugombea tena.

Uchaguzi ndani ya chama hicho utafanyika Juni 29,2024 na yeye atarudisha fomu Juni 20 Mapema katibu wa kamati ya uchaguzi wa chama hicho, Innocent Siriwa amesema mchakato wa kichukua fomu na kurejesha unaendelea hivyo wanachama wajitokeze kugombea.

Aidha amewaasa wagombea wote kufanya kampeni a za kistaarabu huku akiwaonya wale wataoenda kinyume kuwa kuna adhabu

"Kuna Kanuni ambazo zina penati na yoyote atakayeenda kinyume basi ataenguliwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad