HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 15, 2024

POLISI WAUSHUKURU UBALOZI WA USWISI KUFANIKISHA MAFUNZO USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA BODABODA TANGA

Na Mwandishi Wetu,Tanga

JESHI la Polisi Wilaya ya Tanga limetoa shukrani kwa Ubalozi wa Uswisi nchini kwa kuwezesha mradi wa mafunzo ya elimu ya usalama barabara kwa madereva bodaboda wa Jiji la Tanga kwani utasaidia kuondoa changamoto za makosa ya usalama wa barabara.

Shukrani hizo zimetolewa na Mkuu wa usalama wa barabara wilayani Tanga Abel kigai alipokuwa akizungumza wakati wa mafunzo hayo yanayotekelezwa na Amend Tanzania kwa ufadhili wa Uswisi ambapo ameeleza mafunzo yatasaidia kupunguza ajili za barabarani katika Jiji hilo.

Amefafanua kumekuwa na changamoto ya makosa ya barabara yanayofanywa na madereva wa bodaboda ambayo wakati mwingine yanasababisha uvunjifu wa amani ni inatokana na kukosa uwelewa wa sheria.

Ameongeza kuwa kupitia mafunzo hayo wamefundisha elimu ya kuwataka wajiepushe na makosa ya kujichukulia sheria mkononi pale ambapo wanapopata ajali kwa kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kujieupusha na vitendo vya uhalifu inapotokea ajali.

Kwa upande wake Ofisa Miradi Mwandamizi Mratibu kutoka Taasisi ya Amend Ramadhani Nyaza amesema kwamba mpaka sasa wamekwenda madereva bodaboda 180 wakiwa na lengo la kufikia madereva 500.

"Mradi huu ambao unafadhiliwa na ubalozi wa Uswizi unalengo la kuwafikia vijana 750 wanaofanya shughuli za usafirishaji kwa kutumia bodaboda katika mikoa ya Tanga na Dodoma"amesema Nyanza.

Wakati huo huo Diwani wa Kata ya Mabawa Athumani Babu amesema kwamba mradi huo wa elimu utapunguza changamoto ya ajali za barabara kwenye maeneo mbalimbali Jiji Tanga ambapo amesisitiza mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa.

Hata hivyo madereva wa bodaboda waliopatiwa mafunzo walisema kuwa wataweza kuwakuwa mabalozi Wazuri wa kuendeleleza elimu hiyo Kwa wenzao Ili kupunguza changamoto ya uwepo wa ajali za barabara.

"Tunakwenda kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani kupitia shughuli zetu za bodaboda lakini na kuwashawishi wenzetu wengine kuachana na tabia za kujichukulia sheria mkononi lakini na kufuata sheria za usalama barabara "amesema dereva bodaboda Nasib Issa.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad