HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 8, 2024

AFYA NI MTAJI - WOMEN TAPO

KUPITIA Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wajasiriamali pamoja na watanzania kwa ujumla wametakiwa kutumia fursa ya kuwezeshwa kupata matibabu ya afya.

Akizunguma jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Mkurugenzi wa Taasisi ya Women Tapo Lulu Yasini amesema kemp Mbalimbali zinazowekwa kwa ajili ya wananchi zitawawezesha Watanzania kujua Afya zao ha hivyo kujiongezea ufanisi katika kazi zao, akisisitiza kuwa Afya ni mtaji. Kupima na kujua Afya Yako utaweza kupatiwa matibabu kwa haraka na uhakika.

Woman Tapo wamesherehekea siku yao ya wanawake kwa kufanya upimaji wa Bure wakishirikiana na Taasisi Mbalimbali.

Lulu amefafanua kuwa Women Tapo ipo katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anatamani kuona wanawake wakiinuka Kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Tanzania Women Tapo, Lulu Nyapili amesema wanajikita kuelimisha wanawake wanaofanya shuhuli zao sokoni kuwaelimisha kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia, rushwa za ngono, kutambua haki za ardhi na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

Amesema taasisi hiyo ambayo ilianzia Tabata imeanza na kuwafikia wanawake wa Jimbo la Ilala na wanajipambanua kuwafikia wanawake wa mkoa mzima wa Dar es Salaam.na Tanzania kwa ujumla.

Edna Mkono ni miongoni mwa wanamke pata tuzo hizo. Mwanamke huyu ni miongoni mwa wanawake waliyeinuliwa na Tapo hiyo kutoka Tabata kwa kuwezeshwa mtaji na kupata elimu mbalimbali za ujasiriamali alianza kupatiwa mtaji wa elfu 50 na kutokana na elimu aliyoipata sasa mtaji wake umekua na kufikia shilingi laki na nusu.

“Naishukuru sana Tabata Tapo wameniinua walivyonipa mtaji nimeanza kuuza biashara ndogondogo kama karanga, tambi,mkachori na nyingine nyingi.

Mratibu wa Afya kwenye Jamii Dkt.Asha Mahita aliwataka wanawake kuangalia afya zao mara kwa mara kwani mwanamke ni afya

“Mwanamke thamini afya yako kwani afya yako ndio mtaji wako wanawake tuwekeze kwenye afya” amesema

Pamoja na upimaji wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi, wanawake waliofika katika viwanja hivyo walikutana pia na madaktari Mbalimbali wa magonjwa ya Afya ya akili ambayo imeelezwa kuwa wanne kati ya wanawake 10 wanaonekana kuwa na tatizo Hilo.

Kwa upande wao kampuni ya vertex mbao waliratibu zoezi Hilo la upimaji kwa Kushirikiana na hospital ya Aghakhan wametaka Watanzania kutumia fursa ya kuwezeshwa kupata matibabu ya afya kwa wakati .

Akizunguma jijini Dar es Salaam katika viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Meneja wa Kampuni ya Vertex, Herbert Swai amesema vertex ni wadau wa matibabu ya Afya Nchini ambao kwa kutumia kampuni hiyo Mtanzania ataweza kutafutiwa matibabu kwa njia ya haraka hapa Nchi na hata kwenda nchi za nje kama Uturuki, Uingereza, India, Afrika Kusini na nchi zingine kupatiwa matibabu kwa haraka na uhakika na kwa njia ya usalama.

Pia Vertex wanaitangaza Tanzania kwa kuwaalika wagonjwa kutoka nchi jirani kuja katika matibabu katika hospitali za Serikali ikiwemo Muhimbili na Jakaya Kikwete (JKCI) kuja kupata matibabu yao kwa haraka na uharaka na uhakika.

Amefafanua wanahakikisha wanasimamia utaratibu wa kukata tiketi, kupata Viza ya kuja nchini jinsi ya kuweza kupokelewa akifika nchini hata kama mgonjwa anayekuja ni mahututi ataweza kupokelewa kwa njia ya usalama kwa ambulance maalum na maafisa kutoka ndani ya kampuni hiyo.

Kuhakikisha wanasimamia malazi, kuandaa appointment ya kuonana na madaktari bobezi kwakusimamiwa na maafisa kutoka kampuni hiyo.

Amefafanua Vertex inaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii tiba kuitangaza Tanzania kuwa kama kitovu cha matibabu ya afya na kutangaza madaktari wetu bingwa waliopo nchini.

“Tayari tumeshahudumia zaidi ya wagonjwa ya 68 katika huduma hizo kwa kuimarisha afya za watu” amefafanua












No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad