HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 25, 2024

Watanzania Wafunika Kili Marathon


Mgenirasimi Waziri wa michezo na utamaduni Dor Damas Ndumbaro kushoto akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kulimanjaro Nurdin Babu wakitembea km 5 wakielekea katika uwanja wa Chuo kikuu cha ushirika Moshi.
Washiriki wa mbio za kilimita 21 Tigo Half marathon wakikimbia wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana,
Washiriki wa mbio za kilimita 21 Tigo Half marathon wakikimbia wakati
wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliofanyika Moshi mkoani
Kilimanjaro jana.


 Na Mwandishi Wetu 
MBIO za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zimeendelea kuwa kivutio cha watu wengi kiasi cha kufanya shughuli mbalimbali kusimama katika mji wa Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati tukio la 22 la mashindano hayo lilipofanyika leo Februari 25,2024  mjini humobhuku washiriki kutoka Tanzania wakiendelea  kufanya vizuri.

Idadi ya wakimbiaji kutoka ndani na nje ya nchi walishiriki katika mbio hizo ambazo ilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 10,000. Mbo hizo zilijumuisha mbio za Kilimanjaro premium lager 42km, 21km Tigo Half marathon na Gee Soseji 5km fun run.

Sambamba na kuongezeka kwa umaarufu wa mbio hizo, ambazo ni mojawapo ya matukio makubwa ya kimichezo katika Afrika Mashariki, na pia ongezeko la idadi ya washiriki kila mwaka tangu kuanzishwa kwake, kiwango cha mbio hizo kimekuwa kikiongezeka kila mwaka.

Waziri wa Michezo, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro ndiye alienzisha mbio hizo, ambapo pia alishiriki na kumaliza mbio za kilomita 5 za kujifurahisha na baadaye alikuwa kwenye mstari wa kumaliza kupokea washiriki waliomaliza mbio hizo wakiwemo washindi wa vipengele vyote.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Waziri Ndumbaro amewapongeza waandaaji wa mbio hizo ambazo alisema zimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha michezo nchini pamoja na kuibua vipaji vipya kila mwaka.

"Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na waanzilishi wa mbio hizi, pamoja na wadhamini wakuu na wadau wengine wa michezo katika kuhakikisha mbio hizi zilizoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita zinakuwa endelevu kwa manufaa ya maendeleo ya michezo nchini", amesema.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru wadhamini wakuu wa mashindano ya Kilimanjaro premium lager na wadhamini wengine ambao ni pamoja na Tigo- 21km Half Marathon, Gee Soseji – 5Km Fun Run, wadhamini wa meza za maji maeneo wanayopitia wakimbiaji, ambao ni pamoja Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies, Benki ya CRDB na TPC Sugar, pamoja na washirika rasmi amao ni pamoja na Garda World Security, CMC Automobiles, Salinero Hotels na wauzaji - Kibo Palace Hotel na Keys Hotel.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TBL ambao ndio wadhamini wakuu wa hafla hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2003, Michelle Kilpin amesema tukio hilo limepiga hatua kubwa wakati likiingia mwaka wake wa 22.

“Mafanikio haya yameshuhudiwa na mamilioni ya watu duniani kote; imekuwa ni safari ya kusisimua kwani haya ni moja ya mashindano makubwa ya kimataifa ya riadha katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki kwani inawaleta pamoja zaidi ya wakimbiaji 12,000 na watazamaji wengi zaidi kutoka Tanzania na nje ya nchi ambapo mwaka huu ilihusisha washiriki kutoka nchi 56”, amebainisha.

Ameongeza, "Chapa yetu inayotumika katika ufadhili wa tukio hili ambayo ni 'Kilimanjaro' ni jina ambalo linaakisi Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio maarufu duniani; nichukue fursa hii kuwapongeza washindi wote leo na hata ambao hawakushinda lakini walifanikiwa kushiriki mbio hizi”.

Ameendelea kusema kuwa Kilimanjaro Premium Lager imetenga jumla 28m/- kama zawadi kwa jumla, ambapo mshindi wa kwanza kwa mbio za wanaume na wanawake katika mbio za kilomita 42 kila mmoja atajinyakulia shilingi milioni 4 kila mmoja.

Kilpin  pia ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa ushiriiano mkubwa ilioutoa na inaendelea kutoa katika mbio za Kilimanjaro International Marathon katika kipindi cha miaka 22 iliyopita.

“Kama wadhamini wakuu, tutaendelea kuunga mkono tukio hili muhimu la kimichezo ili kuhakikisha sera ya kukuza utalii kupitia michezo inatekelezwa ipasavyo; mafanikio ya tukio hili kupitia ushirikiano wa wadau wengine wa michezo yamesaidia kukuza chapa zetu na kuongeza mauzo ya bidhaa zetu na hivyo kuchangia mafanikio ya kibiashara jambo ambalo limeifanya kampuni ya Bia Tanzania kuwa mlipaji bora wa kodi za serikali na hivyo kutoa mchango mkubwa katika upatikanaji wa ajira na kukua kwa uchumi”, ameongeza.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Innocent Rwetabura kutoka kampuni ya Tigo ambao ni wadhamini wa mbio za Kilimanjaro International Half Marathon alisema, kampuni hiyo inajivunia kuwa sehemu ya mbio za marathon kwa miaka tisa mfululizo na ambazo alisema ni maarufu Barani Afrika.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Gee Soseji ambao ni wadhamini wapya wa mbio za kujifurahisha za Kilomita 5, David Minja, alisema kuwa tukio hilo ni jukwaa sahihi la kuboresha michezo na kwamba kampuni hiyo inajivunia kuwa sehemu ya Familia ya Kilimanjaro Marathon.

“Tutaendelea kushirikiana na wadhamini wakuu, wadhamini wengine na wadau wengine wa riadha katika kuhakikisha tukio hili linakuwa endelevu”, alisema.

Katika mbio hizo, Augustino Sulle kutoka Tanzania ameshinda kitengo cha kilomita 42 kwa wanaume baada ya kutumia saa 02:21:06, mbele ya Abraham Kosgei kutoka Kenya ambaye alitumia saa 02:22:02 na kushika nafasi ya pili, huku Elisha Kimutai pia kutoka Kenya akitumia 02:22:17 na kushinda nafasi ya tatu.

Kwa upande wa wanawake, Natalia Sulle alishinda mbio hizo. Mwanariadha huyo wa Tanzania alitumia muda wa 02:51:23 na kushinda mbio hizo, huku akimtangulia Mtanzania mwenzake Neema Sanka aliyetumia saa 02:51:47, huku Vailet Kidasi akishinda nafasi ya tatu baada ya kukimbia kwa saa 03:01:03 na hivyo kukamilisha ushindi wa Watanzania kwa nafasi zote tatu za kwanza katika kitengo cha kilomita 42 kwa wanawake.

Kwa upande wa wanaume mbio za Tigo Half Marathon, ushindi ulichukuliwa na Faraj Damas kutoka Tanzania aliyetumia saa 01:16:40, akifuatiwa na Peter Mwangi kutoka Kenya aliyekimbia kwa muda wa 01:03:44, huku Mtanzania Kennedy Abel akishika nafasi ya tatu baada ya kukimbia kwa saa 01:04:22.

Kwa upande wa wanawake katika mbio hizo za Tigo Half Marathon zilizotawaliwa na wanariadha wa Kitanzania, Failuna Matanga alishinda mbio hizo baada ya kutumia saa 01:16:40, Neema Kisuda alishika nafasi ya pili baada ya kukimbia kwa muda wa saa 01:16:54, ambapo Neema Mbua pia kutoka Tanzania alishinda nafasi ya tatu baada ya kukimbia kwa saa 01:17:07.

Katika kitengo cha wanawake cha kilomita 21 Tigo Half Marathon, Vivian Opskvik kutoka Norway alikimbia kwa  saa 01:29:09 na kushika nafasi ya 9 jambo amao lilonyesha msisitizo ya kuwa mbio hizo ni za kimataifa.

Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Mbio za Tigo Half Marathon kwa upande wa wanawake Mtanzania, Faulina Mtanga, akimaliza mbio hizo ktika mashindano Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilimanjaro Marathon kelometa 42 Mtanzania kwa upande wa wanawake, Natalia Elisante, akimaliza mbio hizo zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.
Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Mbio za Tigo Half Marathon kwa upande wa
wanaume, Faraja Lazaro, Mtanzania, akimaliza mbio hizo ktika mashindano Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.

Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilimanjaro Marathon kelometa 42 Mtanzania, Augostino Sulle, akimaliza mbio hizo zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.
Watu wa huduma ya kwanza wakitoa msaada kwa mkimbiaji baada ya kupata maumivu ya miguu yake katika mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana,
Mgeni rasimi Waziri wa michezo Dr Damas Ndumbaro kushoto akimkabidhi hundi Sh milioni 50 shindi wa kwanza wa km 42 kwa upande wa wanaume Sulle Augustino katikati kulia Mkurugenzi wa TBL .
Waziri wa Michezo na Utamaduni, Damas Ndumbalo (wa pili kushoto),
akikimbia mbio za kilometa 5 zilizodhaminiwa na Kampuni ya Gee Soseji, katika mashindano ya mashindano ya Kilimanjaro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro jana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad