HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 19, 2024

Tantrade Yachochea Biashara Kati ya Tanzania na Misri

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis akizungumza katika mkutano wa mkakati wa uwekezaji kati Tanzania na Misri uliofanyika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade  Latifa Khamis na Waziri wa Usafirishaji nchini Misri Kamal Al-Waziri mwenye suti ya Samawari  aliongozana na ujumbe'Bluu' jijini Dar es Salaam.

*Yawakaribisha Misri Maonesho ya Biashara Kimataifa

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade) imesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kufungua mipaka imeweza kuonesha fursa kati ya Tanzania na Misri kwenye biashara.

Akizungumza katika Mkutano kati ya Tanzania na Misri Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis amesema ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Misri ni hatua kubwa kuelekea mstakabali bora na ukuaji wa Kiuchumi kwa nchi zote mbili ndivyo inavyoonyesha jinsi nchi za kiafrika zinavyoweza kushirikiana na kukua pamoja.

Mkurugenzi Mkuu katika kuimarika kwa sekta ya biashara Tanzania na Misri zimeona fursa za kujiimarisha na kuongeza thamani kati ya nchi hizo mbili.

Amesema Tanzania huuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani 4,867 huku ikiagiza bidhaa zenye thamani Dola za Kimarekani 49,283 kila mwaka.

Amesema kuwa Tantrade kuwa katika mashirikiano hayo Tantrade inaongeza juhudi kwa kuwezesha biashara kati ya nchi mbili katika kukutana na kujadili na kubadilishana maarifa na kutafuta fursa mpya biashara endelevu

Bi Latifa amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 juhudi nyingi zimefanyika ya kusaidia biashara ndogo ndogo na za kati Tanzania kuuza zaidi ya nje ya nchi na kufikia masoko mapya.

Katika kuonyesha umuhimu wa ushirikiano huo Tantrade imekaribisha kampuni za Misri kushiriki maonesho ya 48 ya Biashara Dar es Salaam.

Maeneo ya Uwekezaji wa Misri katika viwanda vya Dawa,Umeme ,vifaa vya Ujenzi pamoja na Manukato.
Picha ya Pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade  Latifa Khamis na Waziri wa Usafirishaji nchini Misri Kamal Al-Waziri mwenye suti ya Samawari 'Bluu' jijini Dar es Salaam.



Picha za matukio katika Mkutano wa Kibiashara kati ya Tanzania na Misri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad