HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 19, 2024

TANAPA YAANDAA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA NYERERE KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

MAMLAKA za Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Mamalaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wameandaa safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere Machi 2, 2024 katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19, 2024 jijini Dar es Salaam kwa Niaba ya Kamishina wa TANAPA, Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini mwa Tanzania , Asteria Ndaga amesema mtoko huo wa siku moja utahusisha usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam hadi hifadhini na kurudi huku burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali zitatolewa kuanzia kwenye treni hadi kufika.

Aidha amesema kuwa watakaotembelea siku hiyo watapata fursa ya kuingia katika hifadhi na kuona wanayama,ndege,mabwawa mbalimbali na watapata vyakula na vinywaji wakiwa ndani ya hifadhi.

“Lengo ni kuhamasisha wanawake ili kushiriki katika utalii na uhifadhi na umuhimu wake hafla itaanzia Dar es Salaam na kutembelea hifadhi ya taifa Nyerere ili kwenda kuona vivutio mbalimbali vilivyopo na kutoa taarifa za vivutio vya taifa Tanzania na kama TANAPA tunashirikiana wenzetu wa chama cha wanawake wa TAZARA.

Amesema gharama ya mtoko huo kwa mtu mmoja ni Shilingi 200,000 ambapo itahusisha huduma zote ikiwemo usafiri na chakula.

Aidha katika mtoka huo amesema wanatarajiwa kuwafikia zaidi ya wanawake 400 kutoka maeneno mbalimbali huku wanaume pia wakikaribishwa kushiriki.

“Lengo ni kuona uhifadhi unaendelea na kuhamasisha watanzania kupitia siku ya wanawake kila mmoja aone umuhimu na fursa zilizopo katika hifadhi na wanawake katika umoja wetu tukitumia hizo fursa tutaendeleza jitihada za Rais Samia ambaye amejitoa kuhakikisha uhifadhi unaenendlea na kupia filamu ya royal tour tumeongeza wataalii”. Ameeleza

Amesema watakaohudhuria wanatakiwa kujiandikisha kwa kutembelea kurasa za kijamii za TANAPA watapata taarifa zaidi waweze kulipa.

Kwa upande wake dereva wa treni kutoka TAZARA , Bi. Judith Ligenzi amewahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kuona kazi za wanawake wenzao kwani wengine wanasikia kuna madereva wanawake wanaendesha treni na wengine hawaamini.

“Niwahakikishie tupo na tunajiamini na tutaendesha treni kutoka Dar es Salaam hadi Nyerere nakurudi tukiwa salama na tumeona tutengeneze hii kwasababu reli yetu ya TAZARA inapita mbugani na watu watatumia usafiri wa treni ni kilometa 200 kufika eneo la hifadhi.

Amesema katika mtoko huo kutakuwa na wanawake kutoka makundi mbalimba kama taasisi,mashirika,vyuoni na kuwasisitiza wajitokeze kufurahi pamoja kwa kutumia usafiri wa treni na kutembelea hifadhi.

Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini mwa Tanzania , Asteria Ndaga akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Dereva wa treni kutoka TAZARA , Bi.Judith Ligenzi akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Nyerere katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad