Na Mwandishi Wetu,Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Bodi ya TIC Dkt. Benilith Mahenge amefungua rasmi semina ya wafanyabiashara na wawekezaji leo tarehe 18.01.2024 mkoani Kilimanjaro.
Jitihada hizi ni katika kuendelea uhamasishaji wa uwekezaji wa ndani na kuongeza uwelewa kwa watanzania juu ya dhana ya UWEKEZAJI pamoja na kufahamu majukumu ya TIC
Katika kampeni hiyo TIC imejipanga kuratibu semina hizo katika mikoa mbalimbali ili kuongeza uelewa na kuhakikisha watanzania wanafahamu namna maboresho ya sheria mpya ya uwekezaji ya mwaka 2022 chini ya serikali ya awamu ya sita ilivyojikita katika kumkwamua mtanzania kiuchumi
Kwa upande wa washirikinwa semina hiyo Bi. Joyce Ndossi ameshukuru na kusema semina hizi zinaidia sana kuatika kuboresha biashara na uwekezaji hivyo ziwe endelevu ili kuhakikisha jamii inafahamu
Baadhi ya washiriki katika Semina ya Uwekezaji
Mwenyekiti wa Bodi ya TIC Dkt.Benilth Mahenge akizungumza wakati akifungua Semina ya Wafanyabiashara na Wawekezaji
No comments:
Post a Comment