Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
January 31
Jumuiya ya Wazazi wilaya Bagamoyo imeanza Kampeni ya "TUTAKUFIKIA UJIUNGE NA CCM " na kusajili kimtandao ili kuhakikisha ina idadi ya wanachama pamoja na kuwasajili katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Akizindua kampeni hiyo wakati wa maadhimishi ya miaka 47 ya CCM yaliyofanyika Kata ya Zinga ,Mwenyekiti wa Wazazi wilayani Bagamoyo, Aboubakary Mlawa alisema lengo ni kuongeza wanachama .
"Lengo jingine pia kupata takwimu sahihi ya wanachama wa CCM na Jumuiya zake".
Hata hivyo ,Mlawa alisema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu kuwa na takwimu kwa kila Tawi idadi ya wanachama ili kujihakikishia ushindi.
Mlawa aliongeza kuwa kwa aliyofanya Rais Dk .Samia Suluhu Hasan kwa watanzania ,zawadi kwako ni watu kujitokeza na ushindi wa kishindo .
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo , Abdul Rashid Sharif aliwataka makatibu watakaohusika kutoa fomu ,kuachana na tabia ya kuficha fomu na kuwapa wachache wanaowataka kwa maslahi yao.
Alieleza, kila mwanachama anayetimiza vigezo ana ruksa kugombea nafasi za vitongoji na vijiji ,udiwani na ubunge ndani ya wilaya hiyo.
Katika maadhimisho hayo ya CCM miaka 47 kupitia wazazi jumla ya wanachama wapya 70 walijiunga na CCM na kusajiliwa kimtandao na wengine 50 ambao walikuwa hawajasajiliwa walisajiliwa.
Kampeni hiyo ya Tutakufikia Ujiunge na CCM na kukusajili itaendelea katika kata zote wilayani Bagamoyo kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment