HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2024

ATE Mwenyeji wa Mkutano wa Saba wa ASP

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2024 wakati akitambulisha Mkutano wa mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika (ASP) utakaoanza Februari 7 hadi 8 2024 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa saba wa washirika wa Kijamii wa Afrika (ASP) utakaoanza Februari 7 hadi 8 2024 jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2024 Afisa Mtendaji Mkuu wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba amesema jumla ya nchi  50 kutoka barani Afrika zinatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki na mara ya pili kufanyika kwa nchi inayozungumza kiingereza ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika Lagos mwaka 2020.

Amesema kwa ushirikiano wa pamoja na Shirika la Waajiri la Kimataifa (IOE), kwa msaada kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) na Business (ATE) ndio itakuwa mwenyeji wa mkutano huo ambapo pamoja na Mambo mengine,  wadau muhimu kutoka sekta mbali mbali hukutana na kufuatilia maendeleo na changamoto za upatikanaji wa ajira Barani Afrika kote. 

"Washiriki wa mkutano wa mwaka huu watapitia mada muhimu kama mustakabali wa kazi, digitali, maendeleo ya ujuzi wa akili bandia (AI), viwanda na sekta zinazochangia upatikanaji wa ajira Afrika na kutoa fursa ya kipekee ya kupata ufahamu wa mendeleo ya sasa na kushirikiana nyenzo za utendaji bora, ujuzi na kutambua mikakati yenye ufanisi kwa ukuaji endelevu na maendeleo endelevu " amesema Ndomba.

Ameongeza kuwa licha ya utajiri uliopo nchi nyingi za kiafrika zinakabiliana na changamoto kama viwango vya juu vya ukosefu wa ajira , kutokuwa na uwiano wa mapato,  viwango vikubwa vya ajira isiyo rasmi uzalishaji mdogo na mifumo duni ya ulinzi wa kijamii.

Amesema kwa mujibu ya ripoti ya ILO vijana zaidi ya milioni 72 wa Barani Afrika hawapo katika mfumo wa elimu au mafunzo na hawana ajira huku wengi wakiwa ni wanawake vijana.

"Sekta isiyo rasmi inaendelea kudhibiti uchumi wa Afrika na karibu  asilimia 85.5 ya ajira barani humo inachukuliwa kama ajira isiyo rasmi hali inayozuia upatikanaji wa ustawi,  ulinzi wa kijamii na mazingira bora ya kufanyia kazi kwa mamilioni ya wafanyakazi " amesema.

Amesema katika kuhakikisha kunakuwepo na ukuaji wa ajira wenye tija na udhibiti wa kijamii, IOE pamoja na wanachama wake ikiwemo Tanzania wanafanya kazi kwa bidii ili kutatua changamoto hizo kupitia mipango kama mkataba wa washirika wa kijamii wa kiafrika juu ya uumbaji wa Ajira barani Afrika(Blueprint for jobs in Africa).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad