HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 10, 2024

ASKARI WATAKIWA KUJENGA USHIRIKIANO NA WANANCHI




Na Issa Mwadangala

MAOFISA Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Mkoa wa Songwe wametakiwa kuendelea kujenga ushirikiano na wananchi na kutoa huduma bora ili kujenga imani kwa Wananchi wanaowahudumia.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Poisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya wakati alipofanya baraza na askari wa Mkoa huo Januari 10, 2024 wilayani Mbozi ikiwa ni kufanya tathimini na kuweka mkakati hususani kipindi hiki cha mwaka mpya wa 2024.

Kamanda Mallya pia aliwataka askari Polisi wanapotekeleza majukumu yao kuzingatia weledi na uadilifu ili kuleta matokeo chanya ndani ya Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad