Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA)na kupata Maelezo ya kina kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) namna kinavyotambulika kitaifa na kimataifa.
Prof. Mbarawa alitembelea Banda hilo Disemba 6,2023 katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha kuanzia Disemba 5-8, 2023.
Prof. Mbarawa alikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari na kisha kupata maelezo kutoka kwa Godlove Longole Mkuu wa mafunzo ya Uongozaji Ndege ambaye alimweleza namna CATC inavyombulika kitaifa na kimataifa katika upande wa utoaji wa mafunzo ya Usafiri wa Anga pamoja na Mradi mkubwa wa Serikali wa kuboresha Chuo kwa kujenga miundombinu ya CATC ikiwemo majengo mapya yanayoendana na viwango vya Kimataifa.
CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Kwa upande Prof. Mbarawa alisisitiza juu ya umuhimu kuharakisha Ujenzi wa miundombinu ya CATC ambao kwa ujumla wake utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 78 na tayari kwa mwaka huu wa fedha serikali tayari imetenga kiasi cha shilingi Bilioni Tano.
Prof.Mbarawa pia ameitaka TCAA kuendelea kusimamia usalama katika Viwanja vya Ndege nchini hususani kuhakikisha matukio ya ajali za ndege yanadhibitiwa.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kuhusu kuanza ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ili kuweza kuongeza wanafunzi katika chuo hicho wakati wa Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari alipokuwa anaelezea kuhusu Mamlaka hiyo inavyokisimamia Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole alipokuwa anaelezea kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika Mkutano wa 16 wa Wadau kuhusu Ufuatiliaji na Tathmini unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
No comments:
Post a Comment