
Katika hafla Kamishna wa Tira aliipogeza Kampuni hiyo kwa kutoa huduma bora za bima na pia aliwataka wananchi na kampuni zingine za bima kutumia fursa ya uwepo wa sheria, kanuni na miongozo katika kuendelea kuongeza na kukuza shughuli za bima na kukuza uchumi wa wananchi kwa ujumla.
"Mmeainisha dhamira yenu ya “Miaka 25 ya kulinda ndoto zako na kukukinga na majanga ”. Dhamira hii ni nzuri na ndio dira yetu kwenye sekta ya bima.
Ningependa tuidumishe na nitoe rai kwenu na Kampuni zote za Bima, kuhakikisha kwamba jukumu la kukinga majanga nchini linapewa kipaumbele. Hii itakuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Uendelezaji wa Sekta ya Fedha nchini ambapo tunatakiwa kufikisha asilimia ya 50 ya Watanzania wanafikiwa na huduma za bima ifikapo 2023". alisema Kamishna.
Kampuni ya Bima ya Britam Insurance Tanzania Ltd, imekuwa ikitoa huduma za bima zinazowapa wananchi ulinzi wa rasilimali zao, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ustawi wa uchumi. Kampuni hii inahudumia wateja zaidi 47,000 kila mwaka na kulipa kodi serikalini ya takribani shilingi bilioni saba kila mwaka.
Pia Kampuni hii ina matawi katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Mbeya, Mwanza na Arusha pamoja mawakala nchi nzima.

No comments:
Post a Comment