HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 6, 2023

KAMPUNI YA GF AUTOMOBILE YAZINDUA SHOWROOM YA MAGARI YA KISASA NCHINI TANZANIA

   Na Mwandishi Utumishi, Dar Es Salaam

 Kampuni ya uuzaji wamagari madogo  na ya kati ya GF Automobile imezindua duka kubwa la kisasa la uuzaji wa magari  jijini Dar salam ikiwa  ni sambamba na uzinduzi wa gari aina ya Mahindra sokoni 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitilla Mkumbo  alisema ujio wa wawekezaji nchini umetokana na mazingira mazuri ya serikali na ziara zilizofanywa na Rais  Samia Suluhu Hassan katika nchi za Ughaibuni na India ikiawa na lengo la kuwaamasisha makampuni makubwea kuja kuwekeza nchini na sasa leo Tumeona uwekezaji katika sekta ya usafirishaji kwa kampuni ya GF Automobile kuungana na Mahndra na kuingiza magari sokoni

Pia Prof Kitila alisema wao kama watunga sera kupitia Bunge watahakikisha  serikali inapitia upya sera yake ya uagizaji magari kufuatia kuwasili kwa wazalishaji wa magari ya Mahindra kutoka India ili kuwapa nafuu wazalishaji wa ndani na kuvilinda viwanda vyetu naamini hapo baadae tutakuja kuwa na viwanda vingi nchini

Alisema kuwa kampuni ya mahindra na GF Automobile Tanzania wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha sekta ya usafirishaji  ambayo ni injini ya uchumi wa Tanzania.

“Nyote mnakumbuka kuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassana alifanya ziara nchini India hivi karibuni na kusaini Mkataba kadhaa wa Makubaliano (MOU) kwa lengo la kuita na kukaribisha wawekezaji nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GF Automobile Tanzania, Imran Karmal alisema kuwa itaendelea kujitolea katika kuwahudumia Watanzania katika sekta ya Uchukuzi na usafirishaji.

"Tunataka kuihakikishia serikali, washirika, wateja na umma kwa ujumla kwamba tumejitolea kutoa huduma bora ambazo zitaendesha ajenda ya uanzishaji wa viwanda nchini huku akisema kuwa ndani ya kipindi cha miezi 6 kampuni hiyo inatarajia kuunganisha magari hayo nchini Tanzania  na ni uwekezaji unaotarajia kutumia Zaidi ya shilling Bilion 10.," alibainisha.

Mahindra, Mkuu wa Afrika Mashariki na Mahindra Ulaya, Jose Ebenezer alisema kuwa kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 75 ya magari italeta uzoefu, teknolojia, ubunifu katika uhandisi ili kutoa utafiti wa kiwango cha kimataifa wa utengenezaji wa magari nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji ,Prof . Kitila Mkumbo (katikat)na Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya GF Automobile,Mehbooub Karmal(kulia)pamoja na mwakilishi wa kampuni ya Mahndra wakipiga makofi baada ya uzinduzi wa Shoeroom ya magari ya kampuni ya GF Automobile na magari ya Mahndra Dar es salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uwekezaji ,Prof . Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya GF Automobile,Mehbooub Karmal  wakifunua panzia kuashiria uzinduzi wa magari ya Mahndra
Waziri akimkabidhi funguo mmoja ya wateja walinunua gari

Picha ya pamoja ya viongozi wa GF Automobile na Mahndra

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad