Kampuni
ya Ndege Tanzania (ATCL) leo imezindua kampeni ya "Appy Skies"
itakayowazawadia wateja wake wanaotumia "Air Tanzania App" punguzo
maalumu kwenye msimu huu wa sikukuu.
Akizindua Kampeni hiyo Leo
Desemba 1, 2023 jijini Dar es Salaam, Mussa Mbura, Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), amesema uzinduzi wa "Air
Tanzania App" ni muendelezo wa Air Tanzania katika kutumia teknolojia
kwenye kutoa huduma zao.
Mbura amesema Air Tanzania App itasaidia
wateja kupata huduma mbalimbali ikiwemo tiketi, mizigo na kupanga
safari zao kupitia simu zao za mkononi.
"Ulimwengu wa sasa ni wa
teknolojia basi huduma zao nyingi ni lazima ziendane na mahitaji ya
wasafiri wa anga kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma,
kupunguza gharama kwa wasafiri pamoja na kuongeza furaha kwa kutoa
huduma za nyoongeza kwa wateja wa Air Tanzania wanapotumia App hiyo",
amesema Mbura.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mha. Ladislausi
Matindi amesema pamoja na kumiliki soko la anga nchini, Kampuni ya Ndege
Tanzania imeendelea kuboresha huduma zake ili kuongeza furaha kwa wadau
wake haswa wasafiri na watumiaji wa huduma za ndege.
"Air
Tanzania App inamleta msafiri kwenye ulimwengu halisi wa wasafiri wa
anga na kumpa uzoefu wa pekee wa faragha na uhuru wa uchaguzi. Air
Tanzania App sio tu kwa ajili ya kuwezesha safari bali pia inamuwezesha
mteja wa Air Tanzania kunufaika na ofa za bidhaa mbalimbali. Mteja
ataweza kuchagua muda wa safari, daraja la safari, kiti, kununua begi la
ziada mahali popote ulipo, muda wowote anapohitaji kusafiri kwenda.
sehemu yoyote ndani na nje ya nchi ambapo Air Tanzania inafanya safari
zake", amesema Mha. Matindi.
Matindi amefafanua kuwa punguzo hili
ni la asilimia 5 hadi 10 ya bei halisi za tiketi, na ni kwa wateja
wanaokata tiketi zao kupitia "Air Tanzania App" tu ambalo linatolewa
msimu huu wa sikukuu (Holiday Bonus). Mauzo ya tiketi hizo za punguzo
yameanza leo tarehe 1 Desemba 2023 hadi 1 Januari 2024.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa
Serikali Mobhare Matinyi amesema hatua iliyofikiwa ya Air Tanzania kuwa
na App ya safari ni jambo la kujivunia na kufurahia kwa kila Mtanzania
kwa sababu ubora wa huduma unaongezeka ambapo wananchi wataweza kufikia
huduma za tiketi kwa urahisi zaidi, kupata punguzo na nyoongeza ya
huduma mbalimbali zitolewazo kupitia App hiyo.
"Hili ni jambo la
kujivunia, Shirika letu linakwenda kukaa katika mkao wa shughuli hizi za
ndege kimataifa zaidi", amesema Matinyi.
Kampuni ya Ndege Tanzania inatoa huduma kwenye vituo 15 vya ndani ya nchi na 11 nje ya nchi.
Friday, December 1, 2023
Home
Unlabelled
WASAFIRI WATAKAOKATA TIKETI KUPITIA AIR TANZANIA APP KUPATA PUNGUZO LA 5% MSIMU HUU WA SIKUKUU
WASAFIRI WATAKAOKATA TIKETI KUPITIA AIR TANZANIA APP KUPATA PUNGUZO LA 5% MSIMU HUU WA SIKUKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment