HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 1, 2023

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO WA KWANZA WA DIRA YA MAENDELEOYA KITAIFA, KUTOA UJUMBE MAALUMU WA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU

 

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2023 wakati wa kutambulisha rasmi siku ya uzinduzi wa Dira ya Maendeleo ya Kitaifa utakaofanyika Decemba 9, 2023.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jjini Dar es Salaam leo Desemba Mosi, 2023.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa kwanza wa kitaifa wa Dira ya Maendeleo ya Kitaifa utakaofanyika Decemba 9, 2023 katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kutumia siku hiyo kutoa ujumbe maalumu wa kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kuzindua timu kuu ya kitaalamu ya dira pamoja na nyenzo za kidijitali zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wadau.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Desemba Mosi, 2023, Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo amesema kuwa lengo mkutano huo litakuwa ni Kuzindua, Kupokea na kujadili taarifa ya Kitafiti ya tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.

Amesema taarifa ya kitafiti ya tathmini ya Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, imeainisha mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa dira ya taifa ya kwanza ya Taifa ya Maendeleo ambayo ilianza kutekelezwa mwaka 2000 na itafikia mwisho 2025.

Ameeleza kuwa taarifa ya tathmini itaonesha pato la mtanzania ambalo limeongezeka kutoka dola za kimarekani 399.5 ambazo ni shilingi 322,597,000/# kwa mwaka 2000 hafi kufikia dola za Marekani 1200 ambazo ni shilingi 2,880,000/# kwa mwaka 2022.

Pia taarifa hiyo itaonesha utoshelevu wa Chakula kwa asilimia 124 ikilinganishwa na lengo la kufikia asilimia 140 ifikapo 2025, hatua hiyo imewezesha Tanzania kukabiliana na njaa kwa mikoa na wilaya zote nchini.

Mtandao wa barabara za lami na zege katika mikoa umeongezeka kutoka kilomota 4,179 kwa mwaka 2000 hadi kufikia kilomita 11,966.38 kwa mwaka 2023.

Mafanikio mengine ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 760 kwa vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2000 hadi kufikia vifo 104 kwa mwaka 2022 ikiwa lengo limevukwa la kufikia vifo 260 ifikapo 2025.

Pia amesema wadau mbalimbali 971 watahudhuria mkutano huo ikiwa pamoja na viongozi wakuu wa SerIkali ya Muungano wa vyama vya siasa, viongozi wa taasisi za dini viongozi wa taasisi mbalimbali na za sekta binafsi, viongozi wa makundi mbalimbali ya kijamii, yakiwemo wazee, watu wenye ulemavu, wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji madini, jumuiya za kimataifa, wasomi waandishi wa habari.

Wananchi wameombwa na kusisitizwa kufuatilia mchakato wa kuandaa Dira mpya na kushiriki katika kutoa maoni ya kuhusu Tanzania waitakayo miaka ijayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad