HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 20, 2023

Vijana Waaswa Kujadili Changamoto za Kidemokrasia Zinazoikumba Nchi Nyakati za Uchaguzi

 MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba ametoa wito wa vijana kujadili changamoto za kidemokrasia zinazoikumba nchi nyakati za Uchaguzi.


Hayo ameyasema leo Desemba 19, 2023 wakati wa kufungua mafunzo ya Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa nchini, Mafunzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa vijana hao wanatakiwa wajibu changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi Mkuu wa 2020 wa Madiwani, wabunge na Rais.

Amesema kuwa vijana hao wahakikishe wanajadiliana kwa kina miswada mitatu iliyopelekwa katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 11, 2023.

Amesema wajadiliane wakizingatia misingi ya Amani, Haki na mshikamano kwani wao ni wawakilishi wa Mamilioni ya Vijana wenzao kujadili mustakabali wa Taifa kwa ujumla kinapoelekea kipindi cha Uchaguzi wa Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa 2025.

"Ninawaasa kujitambua kwani ni Wakombozi wa Taifa pia mnawawakilisha Mamilioni ya Vijana jadilini kwa kujadili mustakabali wa Taifa." Amewaasa Prof. Lipumba

Kwa Upande wa Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer ametoa rai kwa Viongozi Vijana walioko kwenye Vyama vya Siasa nchini kuhakikisha wanatumia vyema fursa waliyonayo kupigania maslahi ya Vijana wenzao kwenye masuala mbalimbali yanaowahusu kwa kuwa Vijana ndio jicho la Taifa lolote hivyo wanapaswa kuwa makini wanapojadili masuala yanayowahusu.

Pia amewaomba Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa kutumia Mitandao ya Kijamii ili kuwafikia Vijana wengi wanapatikana huko.

Kwa Upande wa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), Zanzibar, Khadija Abdillatif amesema Serikali ya Tanzania inatakiwa kutekeleza takwa la kuanzishwa kwa Baraza la Vijana ili wapate jukwaa halisi wanaloweza kukutana, kujadiliana na kutoka na maamuzi ya pamoja uhusiana na mustakabali wa Vijana na Taifa kwa ujumla.

Kwa Upande wa Mtoa Mada, Deus Kibamba amesema Miswada ya sheria iliyowasilishwa bungeni inamazuri na mabaya katika miswada hiyo.

Amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi wa kitaifa na Sheria ya Uchaguzi Serikali za Mitaa zinaunganishwa na kuwa na sheria moja itakayojulikana kama sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Pia Kibamba amehoji kuhusu Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 1979 inafutwa.? Je Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika chini ya Sheria gani?

"Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa 2023 unaweka takwa la lazima kwa vyama vya siasa kuwa na sera za masuala ya kijinsia."

Pia Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa 2023 unaweka takwa la lazima kwa vyama vya siasa kuhakikisha kwamba nyaraka zake za ndani zinazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Licha ya hayo, Kimbamba ameeleza Mapungufu ya Miswada hiyo kuwa yanakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.

"Wajumbe watatu wenye sifa watakaoteuliwa mmoja akiwa Mwanamke, mmoja mwenye ulemavu na mmoja Kijana wa umri usiozidi miaka 35."

Pia amesema kuwa Masuala mengi yameachwa kwa mfano mgombea binafsi, Matokeo ya Urai kuhojiwa Mahakamani.

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD), Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Desemba 19, 2023 wakati wa kufungua mkutano wa Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Mkurugenzi wa TCD, Bernadetha Kafuko akizungumza katika mkutano wa Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa jijni Dar es Salaam leo Desemba 19, 2023.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer akizungumza katika mkutano wa Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa jijni Dar es Salaam leo Desemba 19, 2023.




Baadhi ya Viongozi wa Vijana wa Vyama vya Siasa wakiwa katika mkutano wa Viongozi wa Vijana wa Vyama vya siasa jijni Dar es Salaam leo Desemba 19, 2023.

Picha za pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad