HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 20, 2023

SH. BILIONI 29 KUSAIDIA KAYA MASKINI- TASAF



Mtaalam wa Mawasiliano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)  Zuhura Mdungi akifafanua baadhi ya mambo katika kikaokazi kati ya Mfuko huo na wahariri wa vyombo vya habari waliokatika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya TASAF Mjombe.
Mchumi wa Mkoa wa Njombe na Mratibu wa TASAF Mussa Selemani akizungumza katika katika kikao kazi kati ya Mfuko huo na wahariri wa vyombo vya habari walio katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya TASAF mkoani  Njombe.
Celina Willson Mhariri kutoka magazeti ya Chama cha Mapinduzi Uhuru na Mzalendo na Mwenyekiti wa Wahariri katika ziara ya kukagua miradi ya TASAF mkoani Njombe akizungumza wakati wa  kikao kazi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF mjini Njombe  Disemba 19, 2023.


Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Mkoa wa Njombe umesema licha ya kusajili kaya masikini 25,585  mkoani humo, hadi Desemba mwaka huu, kaya 709 zimepungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujitoa kwa hiari.

Aidha, imesema kwa kipindi cha Juni na Julai Mkoa huo imetumia Sh bilioni 29 kwa ajili ya kusaidia kaya maskini kupata mahitaji muhimu ikiwemo chakula, mavazi na malazi.

Akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari katika ziara ya kutembelea miradi ya mfuko huo mkoani Njombe leo,   Mchumi wa Mkoa wa Njombe na Mratibu wa TASAF, Mussa Selemani, amesema kuwa kaya za wanufaika wa TASAF zinapungua kadri siku zinavyozidi kwenda.

Selemani amesema kupungua kwa kaya hizo kunatokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi yao kukosa sifa, kuhama bila taarifa pamoja na kujitoa kwa hiari.

Amesema kaya 709 zimepungua na hadi kufikia Desemba mwaka huu zimebaki kaya maskini 24,876.

"Utekelezaji wa mradi wa TASAF Mkoa wa Njombe umegawanyika katika sehemu nne ikiwemo kutoa fedha kwa kaya maskini, kutekeleza  mradi wa kupunguza umaskini, uwezeshaji wa mafunzo kwa vijana wanaotoka katika kaya za wanufaika" amesema Selemani.

Pia amesema kuwa  wanatekeleza mradi maalamu wa kilimo cha parachichi.

Ameeleza kuwa utoaji wa fedha kwa kaya maskini awamu ya tatu ulianza mwaka 2015 na unafanyika kila baada ya miezi miwili kupitia dirisha la malipo.

Ameongeza kuwa malipo ya kaya husimamiwa na kamati za ulinzi wa jamii ambazo zinaundwa na vijiji pamoja na mitaa kwa lengo la kusimamia utekelezaji.

Amesema kuwa katika kipindi cha kwanza cha madirisha 23 ya malipo wametumia Sh bilioni 15.19, huku awamu ya pili wametumia Sh bilioni 13.8.

"Kila mwezi tunatumia shillingi bilioni 29 ni sawa na wastani wa Sh 14,000 kwa kila kaya" ameeleza.

Amesema kuwa mradi wa TASAF umesaidia kuboresha miundombinu muhimu katika sekta ya afya, elimu katika utekelezaji.

Amefafanua kuwa halmashauri zimetekeleza jumla ya miradi 384 ya kupunguza umaskini ambayo zimegharimu jumla ya bilioni 25.6.

Amesema kuwa miradi ya kuboresha miundombinu ilikuwa 191 yenye thamani ya bilioni 19.27, huku mradi wa ajira za muda ikiwa 113 ambao umegharimu Sh bilioni 7.38.

Amebainisha kuwa miradi ya kuongeza kipato ilikuwa 80 ambayo ilitumia Sh bilioni 1.895, huku miradi ya elimu ikiwa 67.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad