NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
MTANDAO
wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa mafunzo kwa Wanaharakati wa jinsia
yenye lengo la kusaidia kuandika shuhuda zao kama kumbukumbu ya matokeo
wanayo yapata wanapo kuwa kazini ili yatumike kuwafunza watu wengine.
Akizungumza
wakati wa mafunzo hayo leo Desemba 27,2023,Mshauri Elekezi wa masuala
ya Maendeleo, Tathimini na Ufatiliaji,Bw.Edson Nyingi amesema kuwa TGNP
imeona kuna haja ya kuandika kuweka kumbukumbu nzuri na ya kudumu na
kuachana na masimulizi pekee kwa njia ya mdomo ili kuweka kumbukumbu.
"Wadau
wengi wa maendeleo wanafanya kazi na matokeo yanapatikana lakini
hapakuwa na namna ya kuweka kumbukumbu za kudumu za matokeo ya kazi hizo
hilo lilionekana swali huko mwanzoni na sasa hivi liko katika
utekelezaji wa kazi za TGNP kuhakikisha inawajengea uwezo wadau wake kwa
matokeo wa kazi wanazozifanya". Amesema Bw.Nyingi
Aidha
ameeleza kuwa wanahitaji kuona matokeo ya kazi wanazofanya wadau wa TGNP
ili kuona jitihada na harakati za kumkomboa mwanamke ili kuwa na usawa
katika masuala ya mgawanyo wa rasilimali na umiliki wa mali.
"Hii
Warsha imelenga katika kuwasaidia wadau kuweza kufatilia taarifa
zinazotokana na hiyo mifumo inayoleta usawa,inayoleta uwiano,katika
masuala ya kijinsia huko kwenye jamii wanakofanya kazi ili kuyafanya sio
tu yawe katika kumbukumbu zao ili yatumike kuwaeleza wengine ili
wajifunze kutokana na matokeo ya kazi zao". Ameeleza.
Amesema
kuna matokeo sasa yanayoonekana kutokana na kazi za Wanaharakati wa
jinsia wa TGNP sasa hivi wanaume wanaongozana na wake zao kwenda kliniki
wanapokuwa wajawazito inatokana na harakati za TGNP za muda mrefu za
kuleta usawa na uwiano wa majukumu katika familia.
Kwa upande
wake, Mwanaharakati wa jinsia kutoka Mkoa wa Kilimanjaro shirika la
Kisonge Community Development Organization Bi.Aika Manase ameishukuru
taasisi ya TGNP kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo ynakwenda kusaidia
kuweka kumbukumbu za kazi inayofanyika katika maandishi ambapo
itachagiza kwa kiasi kikubwa kuweza kuishawishi serikali kuanzia ngazi
ya jamii hadi serikali kuu kuhusiana na mambo yaliyojikita katika mlengo
wa kijinsia.
"Kwa kweli ninalishukuru sana shirika la TGNP
kwa kuandaa mafunzo haya yamekuja wakati sahihi sisi kama mashirika
kwanza tulikuwa tunafanya kazi nzuri, tulikuwa tunawasimulia watu kwa
njia ya mdomo, lakinj mafunzo haya yatatusaidia kama wadau wa maendeleo
kuweka katika maandishi na kuweza kuishawishi serikali katika mambo
yanayohusu Jinsia". Amesema
Bi.Aika amesema sababu ambayo
imesababisha kipindi cha nyuma wasiweke kazi zao katika maandishi ni
uelewa mdogo, ameeleza kwamba kutokana na mafunzo wanayopewa itawasaidia
kuweza kuandika kumbukumbu hata inapotokea mdau wa jinsia amepoteza
maisha wataweza kubaki wengine na kumbukumbu iliyopo kwa njia ya
maandishi.
Naye Dereva Bajaji kutoka katika makundi
yanayopigania Ukombozi,Haki na Usawa wa wanawake Bi.Husna Said ameeleza
kuwa wamepata mafunzo ambayo yataweza kumsaidia kuandika hadithi kwa
ajili ya kumbukumbu ya kazi ambayo ameifanya katika jamii ambayo
itatumika kama chachu ya mabadiliko kwa watu wengine.
Mafunzo
hayo yatakuwa kwa siku nne kuanzia leo Desemba 27-30,2023 ambapo
yamehusisha, Mashirika,Makundi na watu wanaotetea Ukombozi,haki na usawa
wa wanawake nchini.sisha, Mashirika,Makundi na watu wanaotetea
Ukombozi,haki na usawa wa wanawake nchini.
Wednesday, December 27, 2023
Home
Unlabelled
TGNP YATOA MAFUNZO YA KUANDIKA SHUHUDA ZA KUPIGANIA UKOMBOZI,HAKI NA USAWA KWA MAKUNDI MBALIMBALI.
TGNP YATOA MAFUNZO YA KUANDIKA SHUHUDA ZA KUPIGANIA UKOMBOZI,HAKI NA USAWA KWA MAKUNDI MBALIMBALI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment