HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 7, 2023

TCAA YATOA ELIMU KWA WADAU SEKTA YA UCHUKUZI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari amewasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.

Mkutano huo wa siku nne unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ulifunguliwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa umewakutanisha wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, TAMISEMI pamoja na wadau wa sekta ya uchukuzi kutoka sekta binafsi.

Wasilisho hilo limegusa mipango ya Taasisi, mafanikio pamoja na changamoto ambapo wadau walijadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha utendaji ili kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari akiwasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari  (katikati) akijibu maswali ya Wadau wa Uchukuzi wakati wa Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Baadhi ya wadau wa Uchukuzi wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya utendaji ya TCAA iliyokuwa  inawasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari (hayupo pichani) katika Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mussa Mbura akijibu maswali yaliyoulizwakatiaka Mamlaka hiyo wakati wa Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Disemba 5 hadi 8, 2023.
Majadiliano yakiendelea  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad