Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na Jukuu la Wahariri (TEF) na Waandishi wa Habari kuhusiana na mafanikio ya OSHA kwa miaka mitatu ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Jane Mihanji akitoa maelezo kuhusiana na ushiriki wa wahariri katika kikao kati ya OSHA na TEF jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana na uratibu wa Ofisi hiyo kwa Taasisi zilizo chini ya Msajili kueleza juu ya ufanisi wa kazi zao ,jijini Dar es Salaam.
*Lengo ni kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na ajira nchini.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAKALA wa Usalama Mahala Pa kazi (OSHA) imefuta tozo za ada 10 zenye thamani ya Sh.Bilioni 35 ambazo fedha hizo ilikuwa ikipata kila mwaka ikiwa ni kupunguza mzigo kwa wawekezaji kuhusiana na kulipia tozo.
Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda wakati akizungumza katika kikao cha Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Waandishi wa Habari kwa uratibu wa Ofisi ya Masjili wa Hazina kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenda amesema kuwa katika mafanikio ya Miaka mitatu ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan baada kutoa tozo hizo OSHA haijaweza kuteteleka lengo ni kuhakikisha nchi inapata wawekezaji wengi ambao watachochea uchumi na ajira kwa watazania.
"Baada kupunguza na kuondoa baadhi ya ada za huduma ambazo haujaadhiri usimamizi na utoaji wa huduma za usalama wa afya mahali pa kazi nchini," amesema Mwenda.
Amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ya uwekezaji nchini hivyo OSHA kazi yake ni kuendana na Rais katika kuhakikisha adhima ya Rais Wetu inatimia inayoendana na vitendo vya watendaji wake.
Aidha amesema OSHA inaangalia usalama mahala pa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu wameweza kufanya ukaguzi katika maeneo ya kazi yote na kuwapa cheti.
Amesema mafanikio ya Wakala katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 kuhimarika kwa shuhuli za usimamizi mahala pa kazi nchini ambapo wakala amefanikiwa kuongea idadi ya maeneo ya kazi yaliyo sajiliwa kutoka 4336 hadi 30306 ongezeko hilo sawa na asilimia 599.
Mwenda amesema OSHA kwa kushirikiana na wadau wanaanda mpango wa kutambua matumizi ya simu kwenye vituo vya mafuta si salama wanahitaji kutoa elimu zaidi namna ya kuboresha utoaji huduma juu ya malipo ya simu kwenye vituo hivyo.
"Kushirikiana na wadau kutengeneza mpango wa kutambua matumizi ya simu kwenye vituo vya mafuta si salama kwa kutengeneza vibonzo kwa ajili elimu zaidi watu waelewe sii salama kazi yetu kubwa osha ni kuzuia na kutoa elimu, "amesema Mwenda.
Amesema Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya juhudi kuhakikisha kuwa wawekezaji wanakuja kuweza nchini ikiwemo kuhimiza uboreshaji wa mazingira ya biashara kuwa wezeshi na hili ni pamoja na maelekezo mbalimbali katika hotuba zake.
Amesema kuwa wao kama OSHA wamefanya mapitio ya mlolongo wa shughuli zao wa kuweza kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika utoaji wa huduma katika kulinda afya na usalama mahala pa kazi
"Baada yakufanya na kujiridhisha kwa mapitio hayo tukakuta kuna maeneo yanahitaji maboresho ambapo miongoni mwa maeneo yaliyoonekana kuwa na uhitaji wa maboresho tunafanya utatuzi katika kufanya sehemu za kazi zinakuwa salama ili kuwa na uzalishaji wa nguvu kazi unakuwa unatija kwa Taifa".Amesema Mwenda
Amesema ada zilizofutwa ama kupunguzwa na OSHA zimeleta unafuu ambao unachochea ukuaji wa biashara na uwekezaji nchini ikiwemo Kuongeza ajira kwa watanzania.
Ameeleza kuwa kiasi cha ada zilizopunguzwa zinakadiriwa kuwa zaidi ya bilioni 35 ambapo imependeza Rais Dk.Samia fedha hizo zitatumika katika kuhimarisha mifumo ya kulinda wafanyakazi waweze kuzalisha kwa tija.
Hata hivyo amesema idadi ya ukaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104,203 hadi kufikia kaguzi 776,968 sawa na asilimia 646 kaguzi hizo zilizohusisha ukaguzi wa jumla.
Amesema Taasisi ya OSHA amefanikiwa kusimika mfumo wa TEHAMA wa usimamizi wa taarifa za kaguzi nchini ambapo kupitia mfumo huo huduma ya utoaji wa taarifa za ukaguzi ajali na mfumo unafanyika kwa njia ya kieletroniki.
Mwenda akizungumza kuhusu changamoto zinazowakabili amesema baadhi ya waajiri kutotekeleza ipasavyo sheria namba 5 ya usalama na afya mahala pa kazi wanaosimamia ikiwemo kuto wasilisha taarifa za ajali zinazotokea maeneo ya kazi.
Amesema, katiba ya nchi inasema kila binadamu ana haki ya kuishi inatambua hilo na wana program kila maeneo wanafikia kutoa elimu kulinda vijana.
Amesema OSHA imekuwa kimbilio kwa nchi nyingine kujifunza na hiyo kutokana kuwa mifumo thabiti ya utoaji huduma kuwa umetukuka pamoja na kupata kutambulika kimataifa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
No comments:
Post a Comment