HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 21, 2023

MNYAMA ANAKIMBIZA MWIZI KIMYAKIMYA


WEKUNDU wa Msimbazi klabu ya Simba wanaonekana wanakimbiza mwizi kimyakimya kwasasa katika ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo mpaka sasa ameanza kuibua matumaini ya kufanya vizuri tena.

Simba walianza vibaya kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu ambapo hawakufanikiwa kupata ushindi kwenye michezo yao mitatu ya awali, Huku wakilazimika kusubiri mpaka mchezo wa nne ndio wakapata matokeo ya ushindi.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.

Simba wanakimbiza mwizi kimyakimya kweli kwani mpaka sasa wamefanikiwa kukwea kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D, Kwani kabla ya mchezo wa Wydad Casablanca ambapo Simba ndio wamepata ushindi wao wa kwanza klabu hiyo ilikua inashika mkia.

Hauwezi kusema Simba wanafanya vizuri na kuanza kurejesha ubora wao bila kusifia benchi la ufundi la klabu hiyo likiongozwa na kocha Abdelhak Benchikha, Kwani kocha huyo ameonekana kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi hicho kwa kipindi kifupi alichohudumu klabuni hapo.

Simba sasa wamebakiza michezo miwili ambayo inaweza kuwahkikishia kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika, Ambapo mchezo mmoja watakwenda ugenini kukipiga dhidi ya Asec Mimosas na mchezo wa mwisho watakua na faida ya kucheza katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Klabu ya Simba imejiwekea malengo ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika jambo ambalo wamekua wakilipigania kwa misimu takribani mitatu sasa, Japo msimu huu ilionekana kama wasingeweza kufuzu hata hatua ya robo fainali lakini ujio wa kocha Benchikha umeibua matumaini upya.

Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee

ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad