Mnada wa chai kwa mara ya kwanza ulifanyika Tarehe 13 Novemba, 2023 Jijini Dar es Salaam ambapo kwa kipindi chote huko nyuma Chai ya Tanzania ambayo inasifika kwa upekee wa ubora wa blending imekuwa ikiuzwa katika mnada wa Mombasa jambo ambalo limekuwa mwiba kwa wakulima kwani Chai ya Tanzania katika mnada wa Mombasa imekua haipati bei nzuri na hivyo kuwapunguzia wakulima
mapato.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameturuhusu kuanzisha mnada wa chai, ametupatia fedha na kwa kushirikiana wadau wa maendeleo serikali itajenga viwanda vingine Vitano vya kuchakata chai na kukipanua zaidi kiwanda cha Sakare kiweze ku chakata chai nyeusi hasa tukilenga kuwasaidia wakulima wadogo na kuwapa nafasi wakulima wakubwa kupanuka na kuzalisha zaidi katika mashamba yao alisisitiza Bashe, huku akiwapongeza wadau wa maendeleo na watumishi kwa juhudi za kufanikisha mnada huo.
Aidha serikali haitaruhusu uingizwaji wa chai ghafi kutoka nje ya nchi ikiwemo Othordox Tea mbayo kwa miaka yote imekua ikiingizwa nchini kutoka Rwanda. Lengo ni kulinda wakulima wa chai ndani ya nchi kwa kuhakikisha chai yao inapata soko na bei nzuri nchini. Aidha Serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali za kisoko ili kuimarisha mnada wa chai Dar es salaam alisema Mheshimiwa Bashe.




No comments:
Post a Comment