HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2023

Uzinduzi Mpya wa Dar Ceramica Arusha Wawahakikishia Wateja Ubora na Ukaribu

 

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. John Mongella akikata utepe wakati wa uzinduzi upya wa Tawi la Dar Ceramica Centre la Arusha huku wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Mauzo na Masoko, Raymond Nkya (wa pili kushoto) wakishudia.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. John Mongella (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Dar Ceramica Centre, Irene Lyimo wakati wa uzinduzi upya wa Tawi la kampuni hiyo la Arusha. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Masoko, Raymond Nkya.


WAKAZI wa Arusha na miji ya jirani wana sababu za kutabasamu zaidi kufuatia uzinduzi mpya wa Dar Ceramica Centre Tawi la Arusha, ambalo litahakikisha wanapata bidhaa bora zaidi kutoka kwa kampuni inayoongoza katika bidhaa za ujenzi.

Akizindua upya tawi la Arusha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella alikaribisha uzinduzi huo mpya na kusema utaongeza dhamani kubwa kwenye sekta ya ujenzi kwa kuzingatia bidhaa za thamani zinazotolewa na Kituo cha Dar Ceramica chenye chapa bora Afrika Mashariki.

Alisema kama Serikali waliona fahari kuona kampuni za wazawa kama Dar Ceramica zinazomilikiwa na Watanzania zikiku vizuri katika soko la ndani na la kikanda.

“Kuna miradi mingi ya ujenzi inayoendelea Arusha na mikoa jirani kwa sasa kwa kuzingatia kwamba hii ni Geneva ya Afrika,” alisema Mkuu wa Mkoa na kuipongeza kampuni ya ujenzi kwa kuamua kupanua huduma zake kwa kuzindua upya tawi ambalo mwanzoni lilikuwa kwenye Nyumba ya Nobbie Mtaa wa Wapare na lipo katika eneo la Clock Tower, Barabara ya Sokoine mkabala na Benki ya NMB.

Alisisitiza pia ukweli kwamba uzinduzi huo mpya utahakikisha kuna ajira mpya zaidi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wakazi wa Arusha, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya kuwajengea uwezo wa ujuzi na ufahamu wa biadhaa za Kituo cha Dar Ceramica.

“Tunawasihi vijana wetu - wanaume kwa wanawake – kufaidika na uzinduzi huu mpya. Kama kuna fursa za ajira na mafunzo tuzitumie kwa mikono yote miwili,” alisema.

Aliwasihi pia makontrakta wa Arusha na watu binafsi wenye miradi ya ujenzi kununua bidhaa bora kutoka Dar Ceramica kuhakikisha wanapata biadhaa zenye thamani ya pesa.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo mpya, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Dar Ceramica, Bw Raymond Nkya, alisema uzinduzi mpya wa Tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wao wa upanuzi wa huduma nchini kote kuhakikisha Ukanda wa Kaskazini unahudumiwa kikamilifu.

“Sisi ni kampuni inayoona fahari kumilikiwa na Watanzania kwa asilimia 100 na dhamira yetu ni kuhakikisha wateja wetu wote wanapata bidhaa bora baada ya huduma ya mauzo ambayo inawapa watejea dhamani ya pesa wanayostahili,” alisema.

Alisema Kituo cha Dar Ceramica mara zote kimekuwa kikiongoza katika tasnia ya utoaji wa vigae, bidhaa za usafi/udhibiti afya na vifaa vingine vinavyoagizwa kutoka watengenezaji na wasambazi wakubwa Ulaya na China. “Dar Ceramica, ambayo bidhaa zetu zina hadhi ya Superbrand Afrika Mashariki ni kampuni iliyoko Tanzania inayotoa majibu sahihi ya vifaa vya ujenzi kwa wateja wetu Afrika Mashariki na Kati tangu mwaka 1998,” alisema, akiongeza kwamba ubora wa bidhaa zao unafanana nchi nzima.

Alisema wamekuwa wakipokea ushuhuda mwingi kutoka kwa wateja wao mahali wanapotoa vigae, bidhaa za usafi/udhibiti afya na vifaa vingine wanavyoagiza kutoka kwa watengenezaji wakubwa Ulaya na China na ni miongoni mwa sababu kwao kubaki juu katika ubora katika tasnia ya ujenzi kwa takriban miongo mitatu sasa.

Tukio la uzinduzi mpya lililofana sana liliwaleta pamoja viongozi mbalimbali kutoka serikalini Arusha, wafanyabiashara na wateja waliokuwa wamejaa kwenye tawi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad