HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 10, 2023

Chuo cha CATC chafanyiwa kaguzi ya kuidhinishwa na Botswana kuwafundishia wataalam wake wa Usafiri wa Anga

 


Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kimefanyiwa kaguzi na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) yenye lengo la kukiidhinisha kabla ya kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka nchini humo.

 Kaguzi hiyo imefanywa na Mpho Moikwathai Mkuu wa Kitengo cha Utoaji wa Leseni za Usafiri wa Anga nchini Botswana akiambatana na Leabaneng Selawe Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Taarifa za Anga nchini humo tarehe 9 na 10 Novemba, 2023. Kaguzi hizo ni kwa mujibu wa matakwa ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) ambalo linazitaka nchi wanachama kabla ya kupeleka wanafunzi katika vyuo vya usafiri wa anga kufanya ukaguzi na kujiridhisha ubora wake.

Katika kaguzi hiyo, wataalam hao kutoka Botswana wamekagua sifa za chuo katika upande wa ithibati, ubora wa madarasa, ubora wa maktaba, sifa za walimu, mitambo pamoja na nyenzo za kufundishia.

Chuo cha CATC kwa muda mrefu sasa kimekuwa kikipokea wanafunzi kutoka nchini Botswana, baadhi ya nchi nyingine ambazo zinaleta wanafunzi chuoni hapo ni pamoja na Rwanda, Burundi, Uganda, Eswatini, Kenya, Zambia, Guinea Conakry, Msumbiji, Somalia, Namibia, Lesotho na Malawi.Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje akitolea ufafanuzi namna chuo kitakavyokuwa mara baada ya kumalizika kujengwa wakati wa ziara ya viongozi kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) waliofika chuoni hapo kwa ajili ya ukaguzi wa  kuidhinishwa na Botswana kuwafundishia wataalam wake wa Usafiri wa Anga.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje akifanya kikao na wageni kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) waliofika chuoni hapo ili kujiridhisha mazingira kwa ajili ya wanafunzi wanaokuja kujifunza katika chuo hicho
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje (kushoto) akitoa zawadi kwa wageni kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) ambao ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Taarifa za Anga kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB)  Leabaneng Selawe (katikati) pamoja na  Mkuu wa Kitengo cha Utoaji wa Leseni za Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) Mpho Moikwathai.(kulia)
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Taarifa za Anga kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB)  Leabaneng Selawe mara baada ya kutembelea Chuo hicho kwa ajili ya ukaguzi wa  kuidhinishwa na Botswana kuwafundishia wataalam wake wa Usafiri wa Anga.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje (kushoto) akitoa zawadi kwa Mkuu wa Kitengo cha Utoaji wa Leseni za Usafiri wa Anga kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) Mpho Moikwathai (kulia) mara baada ya kutembelea Chuo hicho kwa ajili ya ukaguzi wa  kuidhinishwa na Botswana kuwafundishia wataalam wake wa Usafiri wa Anga.

Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Botswana (CAAB) pamoja na wafanyakazi wa chuo hizo mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad