HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 3, 2023

RC KUNENGE, MATINYI WATETA MAZITO UTEKELEZAJI WA MIRADI YA SERIKALI MKOANI PWANI

 

Msemaji Mkuu wa Serikali na Idara ya Habari MAELEZO Mobhare Matinyi  akielezea jambo kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serikali ndani  Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge  akizungumza   katika mkutano  wa vyombo vya habari  na viongozi  wa Mkoa wa Pwani.

Na Khadija Kalili , Michuzi Tv
IMEELEZWA kuwa Mkoa wa Pwani umepokea kiasi cha Shilingi Trilioni 1.19 katika kipindi cha miaka mitatu cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo zimetolewa mahsusi katika kutekeleza miradi ya mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu , barabara, afya, kilimo na maji.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema hayo leo katika mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Pwani na waandishi wa habari uliohusu utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo uliohudhuriwana mgeni rasmi Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi.

Ambapo pia katika mkutano huo pia umehudhuriwa na wakuu wa wilaya zote pamoja na wakurugenzi wataalamu kutoka idara mbalimbali za serikali Mkoani hapa.

Aidha mkutano huo ambao umefanyika leo Novemba tatu katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Pwani.

RC Kunenge amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo ambazo zimewanufaisha wananchi katika nyanja mbalimbali.

Akizungumza kuhusu suala la migogoro sugu RC Kunenge amesema kwa kila mwananchi ambaye anaona ameonewa katika maamuzi ya eneo alilopo ruhusa aende Mahakamani ili kudai haki lakini kwa upande wake yeye hana mamlaka ya kuingilia mamlaka za serikali zinazosimamia sheria huku akitoa wito kwa wananchi kuacha kuvamia maeneo ya Kambi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
mashamba ya watu binafsi au mipaka ya mikoa huku akiwatahadharisha kuwa sheria ni msumeno.

"Mfano halisi ni uvamizi wa wananchi katika maeneo ya JWTZ ya Msata kambi ya Kihangaiko
,Mafia, Kazimzumbwi huko kote wananchi wavamizi wameshindwa na shauri hili kwa sasa limefikia pazuri na wamekubali hivyo wanasubiri walipwe ili waondoke kwa amani nawasihi wananchi msiingie katika maeneo ya Jeshi kwa sababu yale maeneo yanataratibu zake" amesema Kunenge

Amesema kuwa uchumi wa Mkoa wa Pwani unakua kwa kasi ikilinganishwa na awamu zilizopita kwa sababu hii yote huu ni Mkoa wa mkakati.

"Pwani inakua kwa kasi kwani hivi karibuni mradi mkubwa ambao utakua na njia nne za magari utaanza utakaoanzia Kibaha,Mlandizi na Chalinze jambo ambalo litaufungua Mkoa kiuchumi zaidi" amesems Kunenge.

Katika hatua ingine Wakurugenzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Pwani wametoa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi hiyo ambao ni kutoka majina ya Halmashauri na ya Wakurugenzi kwenye mabano Michael Gwimile (Rufiji) ,Hemed Magano (Kibiti), Beatrice Kwaim (Kisarawe),
Kassim Ndumbo (Mafia), Ramadhan Possi (Chalinze),Waziri Kombo (Mkuranga), Butamo Ndalahwa (Kibaha Vijijini),Mhandisi Mshamu Munde (Kibaha Mji) na Shauri Seleda (Bagamoyo) na Mhandisi Leopold Runji (TARURA) , wakurugenzi wa Halmashauri za hizo za Mkoa wa Pwani, wameeleza namna miradi hiyo ilivyotekekelezwa na kutatua kero na changamoto za wananchi ikiwemo ujenzi wa madarasa ,vyoo na shule zilizojengwa karibu na makazi ya wananchi jambo ambalo limepunguza kwakiwango kikubwa mimba za utotoni na utoro mashuleni wa wanafunzi ndani ya Mkoa wa Pwani.
RC Kunenge amesema ametoa muda kwa Halmashauri ya Mji Kibaha na tayari ameshazungumza na Mkurugenzi wake Mhandisi Mshamu Munde kuhusu kuzungukwa na mapori ambayo yamekua yakimilikiwa na TAMCO na Shirika la Elimu Kibaha bila ya kuyaendeleza huku akisisitiza kuwa Kibaha ndiyo Halmashauri pekee iliyozungukwa na mapori ,amesema tayari amewapa muda maalumu wa utekelezaji na baada ya hapo atachukua hatua.

Awali Msemaji Mkuu wa Serikali na Idara ya Habari MAELEZO Mobhare Matinyi amesema programu hiyo ya kuzunguka nchi nzima kuangalia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini imezinduliwa Novemba mosi mwaka huu Jijini Dodoma jana Novemba 2 2023 imefanyika Mkoani Morogoro , leo Mkoa wa Pwani na kesho itafanyika Jiji la Kibiashara Dar es Salaam na baada ya hapo watakwenda katika Mikoa ya Manyara,Kilimanjaro , Arusha na Tanga.

Ziara hii ya Idara ya Habari MAELEZO inakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo 'Tumewasikia Tumewafikia' ambapo timu ya MAELEZO imezunguka nchi nzima na kurekodi matunda mazuri kwa wananchi ambayo yameshapatikana katika Halmashauri zote nchini ambapo baadaye wananchi watapata fursa ya kuziona katika vipindi maalumu vitakavyooneshwa katika Televisheni ya Taifa TBC na luninga zingine.

"Tutazunguka nchi nzima kuthibitisha kwa wananchi kuwa serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan iko imara imewasikia na imewafikia" amesema Matinyi.
"Kuna pengo tumeliona kwamba wananchi wengi hawana taarifa sahihi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ndiyo sababu iliyotupa msukumo zaidi wa kupeleka waandishi wetu na wapiga picha kuzungukia miradi yote ikiwemo kuzingumza na wananchi kwa ujumla amesema Matinyi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad