HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 7, 2023

COSTECH YAZINDUA KITABU CHA KONGANO

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, akikata utepe kuzindua kitabu cha kongano bunifu chenye lengo la kuwafikia wananchi na kutatua changamoto za kibunifu zinazowakabili katika jamii, hicho Kitabu hicho kilichoandaliwa na COSTECH kwa kushirikiana na serikali ya Sweden na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), kimezinduliwa leo Novemba 7, 2023 jijini Dar es salaam. Katikati ni Afisa Utafiti na Ubunifu kutoka Sweden, Helene Vogelmann na kushoto ni Dkt. , Athuman Mgumia

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha kongano bunifu chenye lengo la kuwafikia wananchi na kutatua changamoto za kibunifu zinazowakabili katika jamii. Kitabu hicho kimezinduliwa leo Novemba 7, 2023 jijini Dar es salaam.
Meneja wa Upatikanaji na Uendelezaji Teknolojia, Athuman Mgumia akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi wa kitabu cha kongano bunifu chenye lengo la kuwafikia wananchi na kutatua changamoto za kibunifu zinazowakabili katika jamii. Kitabu hicho kimezinduliwa leo Novemba 7, 2023 jijini Dar es salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi tv
TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imezindua kitabu cha kongano bunifu chenye lengo la kuwafikia wananchi na kutatua changamoto za kibunifu zinazowakabili katika jamii.

Kitabu hicho kimeandaliwa na COSTECH kwa kushirikiana na serikali ya Sweden na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).

Akizungumza leo Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk Amos Nungu amesema kitabu hicho kina simulizi kutoka katika kongano la mwani Zanzibar, mekanika Morogoro, kilimo cha mpunga na kusaga na kupaki unga kilichopo Morogoro na kimeeleza uzoefu na waliyojifunza.

"Kongano bunifu linawahusu wananchi moja kwa moja. Tunategemea kufasili kitabu hiki kuwa katika maudhui ya Kiswahili," amesema.

Ameeleza kuwa kongano ni mkusanyiko wa watu ambao wanafanya kitu kinachofanana na kwa kupitia wao wanaeleza changamoto zinazowakabili katika kufanya bunifu mbalimbali na kwamba kwa pamoja wnaaweza kufanya vitu mbalimbali.

Kwa upande wake, Meneja wa Upatikanaji na Uendelezaji Teknolojia, Athuman Mgumia amesema kuwa kitabu hicho ni muongozo wa kusaidia watu kufanya ubunifu endelevu.

Amesema tume hiyo ina lengo la kusaidia wabunifu na kwamba ubunifu nchini unafanywa na watafiti kwenye vyuo vikuu, watafiti, watu binafsi na wajasiriamali ambao wako sokoni.

Amesema malengo ya teknolojia ni kuongeza tija na kutimiza mahitaji ya kibiashara zinazozalishwa kuwa na ushindani.

"Wajasiriamali wanafanya bunifu kuhakikisha bidhaa zao zinakuwa shindani sokoni lakini hawana vyanzo vya teknolojia vya kuwafanya wafikie malengo hayo. Tunahitaji watu hawa wakae pamoja ili tuweze kujua teknolojia zinazozalishwa na ziweze kutumiwa ili bidhaa zao ziweze kuuzika sokoni," amesema.

Ameongeza kuwa katika kitabu hicho kuna miongozo zaidi ya mitano ndani yake lengo ni kuweka mazingira ambayo yatawafanya wawe pamoja na kubuni bunifu ambazo zitakuwa na manufaa, kufika sokoni na kutumika.

"Kuna muongozo ambao unaelekeza vitu vya kuwepo ilii wajasiriamali kufanya kazi za ubunifu na kutatua changamoto katika jamii. Pia upo muongozo ambao unawafanya wajasiriamali kufanya kazi pamoja na watafiti na wakati huo huo wakashindana sokoni," ameeleza.

Mgumia amesema "Tunataka kutambua bidhaa wanazozizalisha na wanazitumia katika ushindani ziweze kuingia sokoni na kuleta manufaa nchini."

Mwongozo huo unawalenga zaidi watafiti waliopo vyuoni, wajasiriamali na wafanyakazi wa COSTECH na SIDO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad