Baadhi ya vyeti vya kutambua mchango wa wanaharakati walioisimamisha TGNP Tangu kuanzishwa kwake vilivyotolewa na TGNP katika tamasha 15 jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini na Phumzile Mlambo Ngcuka akizungumza wakati Tamasha la 15 la Sauti ya Pamoja na Miaka 30 ya TGNP lililoambatana na maonesho mbalimbali ya wadau , jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Lihundi akizungumza kuhusiana na Tamasha la 15 la Sauti ya Pamoja na Miaka 30 ya TGNP lililoambatana na maonesho mbalimbali ya wadau , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa TGNP Gemma Akilimali akizungumza kuhusiana na shughuli zilizofanyika na TGNP kwa miaka 30 wakati Tamasha 15 lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vyeti vya kutambua mchango wa wanaharakati walioisimamisha TGNP Tangu kuanzishwa kwake vilivyotolewa na TGNP katika tamasha 15 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya matukio ya picha kwenye Tamasha la 15 la TGNP , jijini Dar es Salaam.
*Akilimali kazi ya Miaka 30 TGNP ndio inaanza
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini na Phumzile Mlambo Ngcuka amesema kuwa wanaharakati wa kifeminia nchini kujikita kuelimisha ulinzi wa mtoto wa kiume kwa mustakabali wa haki na usawa wa jinsia.
Hayo ameyabainisha jijini Dar es Salaam na Phumzile kwenye Tamasha la 15 la Jinsia pamoja na kuadhimisha miaka 30 ya kifeminia la Mtandao wa jinsia nchini (TGNP) linalofanyika viwanja vya TGNP jijini Dar e Salaam.
Amesema katika harakati za kukataa ukandamizaji wa aina yoyote pia suala la ulinzi wa mtoto wa kiume halina budi kuzingatiwa kaa kuendeleza ajenda za kumkomboa kutokana kupitia na changamoto .
"Wanaharakati wa haki za binadamu wasiruhusu aina yoyote ya ukatili kuanzia kuukataa mfumo dume kuanzia katika ngazi ya familia na kuongeza kuwa ipo haja ya kuwepo mabadiliko ya kisera na sheria lakini pia jamii kubadilika," amesema Phumzile.
Amesema ipo haja ya kuwa na majukwaa ya wanaume nchini yenye kueleza yanayowahusu lakini pia yakitumika kuchukua hatua za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaopinga ubaguzi dhidi ya wanawake na wanaokataa ndoa za utotoni.
Amesema mfumo dume sio rafiki kwa wanawake na hata wanaume na umekuwa ukiendeleza ubaguzi hivyo ni muhimu kwa wanaume na watoto wa kiume kuwa miongoni mwa harakati za kuupinga kwani katika karne hii inahitaji wanaume wenye mshikamano na wenza wao.
Aidha amesema tamasha la jinsia litumike pia kuwashirikisha wanaume .
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gema Akilimali amesema licha ya Mtandao huo kuadhimisha miaka 15 za usawa wa kijinsia lakini changamoto bado ni nyingi na mshikamano na serikali unahitajika zaidi kwa sasa kuliko huko walikotoka kwa miaka 30 sasa ndio kazi inaanza.
Amesema katika tamasha hilo la siku nne watatoka na maazimio ya jumla kwani upo mchango wa TGNP katika harakati mbalimbali ziliifanyika
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TNGP, Lilian Liundi amasema Tamasha la jinsia ni jukwaa la kuleta sauti kwa pamoja lenye kujadili kwa pamoja na kupanga mikakati.
"Tamasha hili ni la 15 tangu kuanzishwa limeweza kuwa na washiriki 2000 hadi 5000 kwa tamasha moja limewafikia watu zaidi ya 35000,"amesema Liundi.
Amesema tamasha hilo limewaleta watu kwa pamoja ukanda wa Afrika na wameendelea kusimama kwenye misingi ya wasisi wao.
Aidha amesema TGNP imejengwa katika misingi imara ya haki na kuondoa mifumo kandamizi.
No comments:
Post a Comment