Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo na Mtafiti Chuo Kikuu Mzumbe Aloyce Gervas wakikabihi jezzi kwa wanakikundi cha Five Star Jogging
cha Tandale akipokea ni Mwenyekiti wa Five Star Jogging Tandale, Ramadhani Abdala Juma.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza leo Novemba 10, 2023 wakati wa kutoa elimu juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wanakikundi cha Five Star joggin kilichopo Tandale jijini Dar Es Salaam.
Mtafiti Chuo Kikuu Mzumbe Aloyce Gervas akizungumza na akizungumza leo Novemba 10, 2023 wakati wa kutoa elimu juu ya Hifadhi za jamii kwa wafanyakazi wa sekta zisizo rami kwa wanakikundi cha Five Star joggin kilichopo Tandale jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Five Star Jogging Tandale, Ramadhani Abdala Juma akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa Jezi ambazo watazitumia kufanya mazoezi nakuhamasishana kuwa na maadili mema.
Picha za pamoja.
Wanakikundi cha Five Star Jogging Tandale wakijaza fomu kwaajili ya kujiunga na Mfuko wa Hifadhi za jamii wa NSSF
Wafanyakazi wa NSSF wakitoa elimu kwa Wanakikundi cha Five Star Jogging Tandale
Matukio mbalimbali.
Na Mwandishi wetu.
UELEWA mdogo ma kipato kidogo, vimetajwa kuwa ndio changamoto ya watu wasio katika mfumo rasmi wa ajira kujiunga na mifuko ya hifadhi za kijamii pamoja na bima za afya nchini.Hayo yamesemwa na Mhadhiri na mtafiti wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo leo Novemba 10, 2023 wakati wakitoa elimu kwa vijana kikundi cha mikimbio mwendo (Jogging) ya Five Star iliyopo Yemeni Tandale wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe Kinatoa Elimu kupitia tafiti iliyofanyika katika nchi tatu ikisusisha Chuo cha Nairobi nchini Kenya, Chuo Kikuu Mzumbe na Roskilde.
Amesema utafiti huo ulijikita katika huduma ambazo Wajasiliamali wadogo wanatakiwa kuchangia ambazo ni Pensheni za Mifuko wa Hifadhi za jamii (NSSF), Bima ya Afya, Mikopo ya Biashara ya Benki na Saccoss, Mafunzo ya Veta, NIT na Polisi. Pamoja na huduma ya Ushirikishwaji wa Vikundi, vyama vya wafanyakazi...
Amesema kuwa Kikundi cha Five Star Jogging hawana uelewa kuwa wanaweza kupata Pensheni ya Uzeeni kwani wanajua kama Pensheni inapatikana kwa Wafanyakazi wa Serikalini tuu, hivyo katika kuwapa elimu baadhi ya wanakikundi hicho wamejaza fomu kwaajili ya kuanza kuchangia.
"Sisi Chuo Kikuu Mzumbe katika Utafiti wetu tumeenda mtaani kabisa kuangalia hawa watu wanajikimu namna gani na namna ambavyo wanaweza kujikimu katika maisha yao. Mzumbe tumeazimia kwenda Mtaani, Mtaa kwa Mtaa kuamsha watu kuhusu hizi hifadhi za jamii." Amesema Dkt. Kinyondo.
Makundi ambayo yameshafikiwa ni Wajasiliamali wadogo, Bodaboda, Makondakta, Wajenzi, Mama Ntilie na vikundi vya Jogging.
Akito ushauri kwa NSSF, amesema kuwa watumie ukuaji wa teknolojia katika kutoa huduma ili kuondoa usumbufu kwa jamii pale inapofatilia Mafao yao pale wanapohitaji mafao au wanapostaafu na nguvu kupungua.
Pia amewaasa wana Kikundi cha Tandale Five Star Jogging kukata bima ya Afya ili iweze kuwasaidia pale waapata Changamoto za kiafya.
Dkt. Kinyondo ameeleza kuwa nchi inapoenda kuwa na bima ya wote, ni wajibu wa kila mwananchi kujibidisha kushiriki kwani kuna nchi ambazo zilishatekeleza mpango huo mfano Rwanda na Ghana. Hata hivyo ni asilimia isiyozidi 60 wamejiunga huko Ghana, na Rwanda ni kama 80 wamejiunga.
Hivyo elimu inahitajika kwa wananchi kupokea mpango wa Bima ya afya kwa wote. Ila katika tafiti imegundulika kwamba wafanyakazi wa sio katika sekta rasmi muda wao ni kutafuta kipato hivyo hawataki urasimu kwenye huduma. Hivyo utegemea zaidi kulipa fedha toka mifukoni huko hospitali wakiamini ukiwa na hela unatibiwa haraka kuliko ukiwa na bima.
Pia wamelalamikia suala la kukosa dawa hospitali pale wanapopata huduma kwa kutumia bima ya afya.
Akizungumzia kuhusiana na kuwekeza amesema Uwekezaji katika mfuko wa UTT unafaida kwani unaweka fedha na pia unapata faida. Amesema kuwa vikundi vingi walivyovifikia, vimeweza kujiunga na UTT na ameshauri kikundi hiki kujiunga na mfuko huo, jambo ambalo wamekubaliana kulishughulikia hilo wiki ijayo.
Kwa Upande wa Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas amewakumbusha kudumisha umoja walionao ili kuwezakufika mbali ikiwa pamoja na kuomba mikopo mbalimbali itakayowawezesha kufanya biashara.
"Kidole Kimoja hakivunji Chawa ushirikiano ni mzuri na unaleta maendeleo kwa haraka zaidi kuliko ukiwa peke yako," amesema Aloyce.
Amesema amewaasa kuheshimiana wawapo kwenye kikundi wadumishe upendo na ushirikiano hapo hakuna kitu kinachoharibika na ili kikundi kisonge mbele.
Licha ya Kutoa elimu kuhusu Mifuko ya Kijamii Wametoa jezi za Kikundi chao ambazo watatumia wakati wa kufanya mazoezi.
Licha ya hayo Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Tafiti amesema watawafikia vikundi vingine ambavyo vitakuwa balozi wa kueneza hifadhi za jamii kwa wananchi katika maeneo wanapoishi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Five Star Jogging Tandale, Ramadhani Abdala Juma amewashukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa Jezi ambazo watazitumia kufanya mazoezi na kuhamasishana kuwa na maadili mema.
Amesema kuwa changamoto kubwa ilikuwa ni namna ya kupata bima za afya na Mifuko ya Pensheni. "Hivyo basi wametupa elimu ya namna ya kujiunga na mifuko ya kijamii na bima ya afya katika vikundi vidogo vidogo tulivyonavyo, jambo jingine ni kutokujua kama wanajogging pia wanaweza kupata Pensheni Uzeeni pamoja na bima ya afya."
Pia amewaahidi Chuo Kikuu Mzumbe kuzitumia Jezi hizo kwa maadili bila kuaibisha nembo au Chuo Kikuu Mzumbe.
No comments:
Post a Comment