HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 13, 2023

ZAWADI ZATANGAZWA KWA WASHINDI WA ATLAS HALF MARATHON 2023


Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akitambulisha zawadi za washindi wa mbio za Kilomita 5 kwa watoto, kilomita 10 na 21 kwa watu wazima. 

Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper akionesha baadhi ya Vibali kwaajili ya Atlas Half Marathon itakayofanyika kesho Oktoba 14, 2023 ambapo wamejikita katika kutokomeza Ukatili dhidi ya watoto.

Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper akionesha moja ya Fulana zitakazo tumika kesho Oktoba 14, 2023 wakati wa mbio za Shule za Atlas.
Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper akionesha medali za washindi watakaoshiriki mbio za Atlas Kesho Oktoba 14, 2023.
Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper akionesha namba zitakazotumika kesho kwenye Mbio za Shule za Atlas.


Baadhi ya wadhamini wakifafanua namna watakavyoshiriki katika mbio za Shule za Atlas kesho Oktoba 14, 2023.

KUELEKEA siku ya Atlas half Marathon 2023 Shule za Atlas waweka hadharani zawadi za washindi katika mbio zitakazofanyika kesho Oktoba 14, 2023 kuanzia shuleni Atlas Madale jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wakutambulisha zawadi hizo kwa washindi mbalimbali, Mwalimu kutoka Shule za Atlas, Willbroad Prosper amesema kuwa Atlas Half Marathon ya kesho itakuwa kivingine kwani watakuwa wanakauli mbiu isemayo, "Tokomeza Ukatili dhidi ya Watoto" ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwalinda watoto dhidi ya ukatili.

Amesema kutakuwa na zawadi kwa Msindi wa kwanza mpaka mshindi watano kwa jinsia zote watakao shiriki kuanzia kilomita 10 na kilomita 21. Pia kutakuwa na zawadi maalumu kwa watoto jinsia zote kuanzia mshindi wa kwanza hadi watano watakao shiriki mbio za kilomita 5.

Kwa watoto zawadi kwamshindi wa kwanza wa mbio za kilomita tano atapata shilingi 300,000#, mshindi wa pili shilingi 250,000#, Mshindi wa tatu atapata shilingi 200,000#, Mshindi wa nne atapata shilingi 150,000#,Mshindi wa tano atapata shilingi 100,000#. zawadi hizo ni kwa jinsia zote.

Kwa upande wa Watu wazima watakao shiriki mbio za kilomita 10, Wanawake Mshindi wa kwanza atapata shilingi 250,000#, wapili, shilingi 200,000#, watatu shilingi 150,000#, wanne 100,000# na watano shilingi 75,000#. Kwa upande wa Wanaume Mshindi wa kwanza atapata shilingi 200,000#, wapili, shilingi 150,000#, watatu shilingi 100,000#, wanne 75, 000# na watano shilingi 50,000#.

Na Kwa wandishi wa kilomita 21 kwa watu wazima Wanawake Mshindi wa kwanza atapata shilingi 200,000#, wapili, shilingi 150,000#, watatu shilingi 100,000#, wanne 75,000# na watano shilingi 50,000#. Kwa upande wa Wanaume Mshindi wa kwanza atapata shilingi 200,000#, wapili, shilingi 150,000#, watatu shilingi 100,000#, wanne 75, 000# na watano shilingi 50,000#.

Prosper amesema kuwa Maratho ya mwaa huu imeboreshwa zaidi kwani wanavifaa vizuri kwaajili ya washiriki huku wakiwa na lengo la kutokomeza ukatili katika jamiik hasa watoto. Amesema Pia katika medai na flana za mwaka huu zina ujumbe wa kutokomeza ukatili dhidi ya Watoto.

Hivyo wametoa wito kwa jamii kujisajili mapema kabla muda hauja fungwa Leo Oktoba 13, 2023 saa mbili usiku.

KwaUpande wa Katibu wa Chama Cha riadha Tanzania, Samwel Mwela amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika hivyo wananchi na wadau wote wajitokeze katika kushiriki marathoni ya shule za Atlas itakayofanyika kesho Oktoba 14, 2023 ambayo ni Nyerere Day kuanzia saa 11:30 mpaka saa 4:30 asubuhi kuanzia njia ya Goba Madale katika Shule ya Atlas Madale kwa msimu wa Tano Mfululizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad