HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 16, 2023

WATU WATATU MBARONI KWA TUHUMA YA MAUAJI

 NA DENIS MLOWE, SUMBAWANGAJESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Baraka Markusi Nyangala (30) mfanyabiashara mkazi wa mtaa wa Kasisiwe Manispaa ya Sumbawanga.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP, Shadrack Masija alisema kuwa Watuhumiwa hao walimuuwa kwa kumpiga na Rungu kichwani kisha kuchimba shimo na kumfukia akiwa hai.

ACP Masija akizungumzia tukio Hilo alisema kuwa Watuhumiwa hao wa mauaji walifanya tukio Hilo Septemba 28 mwaka huu baada ya kumpigia simu marehemu kumjulisha kuwa kuna maharage wanauza.

Alisema kuwa baada ya kukubaliana alikwenda kijiji Cha Katazi wilaya ya Kalambo kwa ajili ya kununua maharage wakiwa wote wanne ndipo walipofika porini walitimiza Nia Yao ya kumpiga Rungu kichwani.

Alisema kuwa Marehemu akiwa na Watuhumiwa hao walifanikiwa kumnyang’anya fedha Tsh 1,840,000 pamoja na pikipiki na baada ya kitendo hicho walichimba shimo na kumfukia akiwa hai.

Aliongeza kuwa Taarifa ya kupotea kwa Baraka Nyangala zilifika polisi na ndipo Uchunguzi ulifanyika kwa kuwatumia intelejensia na wataalamu wa cyber crime na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao wakaongoza mpaka eneo walilomfukia marehemu.

Alisema kuwa lengo la tukio Hilo ni unyang'anyi wa Mali kutoka kwa marehemu na kutoa wito kwa jamii kuacha tamaa za kupata utajiri au Mali
za haraka haraka pasipo kufanya kazi halali.

Aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Frank Simsokwe (33) , Edfonsi Simsokwe (28) na Niikas Lunguya (38) ambao baada ya kuhojiwa walikiri na kwenda kuonyesha eneo walilomfukia.

Katika tukio jingine Kamanda Masija alisema kuwa mahakama ya wilaya ya Nkasi imemuhukumu Mariam Misango (43) mkulima mkazi wa Isale wilayani Nkasi kifungo Cha miaka 5 kwa kosa la kuiba mtoto mchanga mwenye masaa matatu baada ya kuzaliwa na mama yake Ednatha Mwendapole.

alisema tukio Hilo lilitokea tarehe Septemba 22 mwaka huu majira ya saa 6.30 alasiri katika hospital teule ya wilaya ya Nkasi

Alisema kuwa mama huyo alimlaghai mama wa mtoto kuwa anampeleka mtoto kupata chanjo ya Polio Kisha akatoweka naye kusikojulikana hivyo alitiwa hatiani kwa kosa la wizi wa mtoto mbele ya hakimu mkazi Denis Luwango.

Kamanda Masija alitoa wito kwa kwa akinamama wasio na watoto ni vema waende hospitalini wapate vipimo wajue ni nini kinasababisha wasibebe ujauzito kuliko kujiingiza kwenye uhalifu wa kuiba watoto Kwani wakibainika adhabu yake ni kufungwa jela.

Aidha alitoa wito kwa Wananchi waendelee kutoa taarifa zinazohusiana na uhalifu na wahailifu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Shadrack Masija 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad