HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 16, 2023

Mkazi wa Songea ashinda pikipiki kupitia droo ya Kopa Tukubusti ya Benki ya Letshego Faidika

 
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Mkazi wa Ruvuma, James Chiwangu ameshinda pikipiki aina ya boxer kupitia droo ya kampeni ya mpya ya Kopa Tukubusti ya benki mpya ya kisasa nchini, Letshego Faidika.

Chiwangu alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kushinda pikipiki katika droo hiyo ambayo malengo yake makubwa ni kuwawezesha wateja wa benki hiyo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

“Najisikia fahari kubwa sana kushinda pilipiki kupitia mkopo wangu. Nimeweza kupewa mkopo ambao umeniwezesha kunisaidia katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii na kupitia mkopo huo, nimeshinda pikipiki pia,” alisema Chiwangu.

Mbali ya Chiwangu ambaye ambaye ni mfanyakazi wa Halmashauri ya mkoa wa Ruvuma, pia benki ya Letshego Faidika imetangaza washindi wengine wanne wa kampeni hiyo ambayo lengo lake ni kuwawezesha wateja wao ambapo ushinda asilimia 50 ya kiasi cha fedha waliyokopa.

Washindi hao ni Ismail Lugenge, mkazi wa Liwale mkoa wa Lindi aliyeshinda sh 103,000 , Lutende Sospeter wa Kibondo, mkoani Kigoma ambaye ameshinda kiasi cha Sh100,000 na Joyce Mshana pia wa Kibondo aliyeshinda kiasi cha Sh228,034.

Pia katika orodha hiyo ni Ibrahim Jalala ambaye ameshinda kiasi cha sh925,772 kupitia droo hiyo na kufikisha jumla washindi 10 waliofadika na kampeni hiyo mpaka sasa.

Kwa upande wake, meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa aliwaomba wateja wao kuchangamkia mikopo yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kuweza kusaidia kugharimia mahitaji mbalimbali.

Nalingigwa alisema kuwa bado washindi 20 ili kukamilisha kampeni hiyo mwezi Desemba mwaka huu na kuwaomba wateja wao kuendelea kukopa na kuingia kwenye droo hiyo. Benki hoyo imetenga kiasi cha Sh50 billion kwa ajili ya kuwazawadia wateja wao kupitia kampeni hiyo.

“Tumeweka jumla ya Sh50 biliioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti. Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu. Kwa mfano, mteja anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh milioni 150 ambapo akishinda kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75,” alisema Bw. Nalingigwa.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru aliipongeza benki ya Letshego Faidika kwa kuendesha droo hiyo ambayo inawafaidisha wateja wake.

Mfuru alisema kuwa droo hiyo imekidhi vigezo vyote na kuwaomba wateja wa benko hiyo kuchangamkia fursa hiyo ili kunufaika nayo.

Meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) akizungumza wakati wa droo ya kutafuta washindi watano wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao. Kulia ni Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru.

Meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (kulia) NA Afisa Msimamizi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Pendo Mfuru wakimsikiliza kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa kampeni Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao.

Meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa akimsikiliza kwa njia ya simu mmoja wa washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lengo la kuwafaidisha wateja wao.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad