HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 2, 2023

Wateja watano washinda fedha kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti ya benki ya Letshego Faidika

 Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Wateja wa Benki ya Letshego Faidika wameanza kufaidika na kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la KOPA TUKUBUSTI baada ya kushindia zawadi za fedha katika droo ya kwanza.

Katika droo iliyofanyika leo Oktoba 2, 2023, jumla ya washindi watano wameshinda fedha kupitia mikopo yao katika benki hiyo.

Washindi hao ni, Justine Taabu ambaye ni mfanyakazi katika Jeshi la Magereza, alijishindia Sh354,500 wakati Nghoyelwa Magadula wa Mwanza alishinda sh 815,000 na Egifredi Chihakuchao wa Morogoro alishinda sh 399,465.

Washindi wengine ni Ngwamba Maugira wa Mwanza ambaye alishinda Sh432, 207 na Bahati Mlenda alishinda kiasi cha Sh107, 602 na kuifanya benki hiyo kutumia Sh2, 108,774 kuwazadia washindi hao. Zoezi la kupata washindi hao lilisimamiwa na Bw Joram Mtafya kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha

Akuzungumza mara baada ya kutangaza washindi hao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika Bw Baraka Munisi alisema kuwa lengo kubwa ya kampeni hiyo ni kuwafaidisha wateja wao na sasa wamebakiza jumla ya washindi 25 ili kumaliza kampeni hiyo.

Bw Munisi alisema kuwa wamtenga jumla ya Sh50 billioni kwa ajili ya kukopesha wateja wao. Alisema kuwa kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, mteja anaweza kushinda fedha kiasi chochote kutegemea na fedha aliyokopa.

“Tumeweka jumla ya Sh50 biliioni kwa ajili ya kukopesha wateja wetu. Mteja anaweza kushinda fedha ya ziada (Bonus) ya asilimia 50 ya kiasi cha fedha alichokopa kupitia kampeni hii mpya ya Kopa Tukubusti. Lengo hapa ni kubadili maisha ya wateja wetu” alisema Bw. Munisi.

Alisema kuwa mteja wao anaweza kukopa mpaka kiasi cha Sh milioni 150 ambapo akishinda kupitia kampeni ya Kopa Tukubusti, atazawadiwa Sh milioni 75.

Kwa upande wake, meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa alisema kuwa watafanya droo ya washindi kila baada ya wiki mbili na kuwaomba wateja wao kuchangamkia kampeni hiyo ili kushinda zawadi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Bw Nalingigwa, vigezo mbalimbali vimewekwa kwa washiriki wa kampeni hii ikiwa pamoja na umri kuanzia miaka 18, lazima awe mfanyakazi aliyethibitishwa wa serikali na taasisi binafsi na lazima awe na sifa za kupata mkopo kwa mujibu wa vigezo na masharti.

Kwa upande wake, mmoja wa washindi wa Bw. Justine Taabu aliipongeza benki hiyo kwa kuanzisha kampeni hiyo ambayo inasaidia kupata fedha za ziada ili kukidhi mahitaji yao mbalimbali.

“Nimefarijika kushinda, kwa kweli Benki ya Letshego Faidika mnastahili pongezi kwa ubunifu huu wenye tija kwa wateja, fedha hizi ziatasaidia kutatua changamoto mbalimbali, nawaomba wafanyakazi wa serikali na taasisi binafsi, kujiunga na benki hii,” alisema Bw. Taabu.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika, Bw Baraka Munisi akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti yenye lango la kusaidia wateja wao.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika, Bw Baraka Munisi (wa pili kushoto) akishuhudia jinsi droo ya kusaka washindi wa kampeni ya Kopa Tukubusti ikichezeswa. Anayeshuhudia zoezi hili hilo ni meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw. Asupya Nalingigwa (wa kwanza kushoto) na pili kulia ni Joram Mtafya kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha na wa tatu ni afisa wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano wa kampuni ya Radian Limited Kundani Makimu.

Afisa msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Joram Mtafya (wa kwanza kulia) akishuhudia zoezi la kutafuta washindi wa kampeni ya Kopa Tukuvusti ya Benki ya Letshego Faidika. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Letshego Faidika na wa kwanza kushoto ni meneja Masoko na Mauzo wa benki ya Letshego Faidika Bw Asupya Nalingigwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad