HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 2, 2023

USHIRIKIANO KATI YA MUHAS NA SWEDEN WANUFAISHA WATAFITI 95 TANZANIA

 


Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Marcias na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS Profesa Aporinary Kamuhabwa wakikata utepe kuzindua na kituo cha ubunifu maeneo yote katika chuo cha MUHAS Mloganzila jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2, 2023.   
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Marcias na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS Profesa Aporinary Kamuhabwa  wakikata utepe kuzindua maabara ya Biorepository jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2, 2023.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WATAFITI 95 ngazi ya uzamivu kutoka Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) wamefaidika katika tafiti na mafunzo kupitia ufadhili kutoka shirika la maendelea la Sweden(SIDA).

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS Profesa Aporinary Kamuhabwa amesema hayo leo Oktoba 2,2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha miaka 47 ya ushirikiano kati ya MUHAS na Sweden kupitia SIDA na miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden

Pia wakati wa maadhimisho hayo Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Ozaki Marcias amezindua maabara ya Biorepository na kituo cha ubunifu maeneo yote katika chuo cha MUHAS Mloganzila.

Profesa Kamuhabwa amesema, walianzisha ushirikiano huo kwa lengo la kusaidia tafiti na mafunzo kama vile VVU/UKIMWI, kifua kikuu na malaria na kuongeza kuwa zilichangia kutoweka kwa sera ya nchi.

"Sisi kama Chuo Kikuu cha Afya tafiti zetu na mafunzo yetu ziko kwa upande wa Afya na Sayansi Shirikishi, watafiti hawa wamesoma kwa njia za kufanya tafiti hivyo kupitia Sida tumefanya tafiti nyingi zikiwemo za magonjwa ya kuambukiza ambapo mwanzoni tulianza na ukimwi, kifua kikuu na malaria na magonjwa mengine".

Amesema siku hizi magonjwa yanazidi kubadilika, na kuna magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo mpango unaoendelea sasa ni kufanya tafiti katika magonjwa yasiyoambukiza na kuja na matokeo chanya.

"Chuo cha MUHAS ni Chuo cha tatu kwa ukubwa katika nchi ziliopo chini ya Jangwa la Sahara, hivyo mnaweza mkaona ushirikiano kama huu unafanya chuo kuweza kutambulika Kimataifa lakini tafiti ambazo zimefanyika kwa kushirikiana na MUHAS zimeweza kutoa majibu yanayolenga kutatua matatizo na changamoto za wananchi" amesema Kamuhabwa

Profesa Kamuhabwa ameongeza kuwa, ushirikiano huo pia umeiwezesha Muhas kupata, teknolojia mpya zaidi huku tafiti zake zimechangia sana mabadiliko ya dawa haswa zile za malaria.

Wakati wa Covid-19, MUHAS ilifanya utafiti juu ya chanjo, dawa na kinga
Ameongeza kuwa, mpango ulikuwepo wa mashirikiano kati ya Sida na MUHAS wa 2015 unaenda kufikia ukingani na wanatarajia kuingia makubaliano mapya ambayo yanatarijiwa kusainiwa Novemba mwaka huu.

Amesema mpango huo utakaodumu hadi mpaka 2026 utakuwa ni muendelezo wa kuendelea kutoa mafunzo kwa wanataaluma na kufanya tafiti.

Kwa upande wake balozi wa Sweden nchini Tanzania Marcias mesema, Tanzania na Sweden zimeshirikiana kwa miaka 47 katika masuala ya VVU na Malaria na kwamba serikali yake kupitia SIDA imeisaidia MUHAS jumla ya dola za kimarekani bilioni 90 tangu kusainiwa kwa ushirikiano huo.

"Mafanikio makubwa yamepatikana hadi sasa na tunathibitisha hilo, ninatarajia kuona kwamba tunatia saini awamu mpya ya ushirikiano," amesema

Naye Profesa Eligius Lyamuya wa Microbiology na Immunoology kutoka MUHAS amesema kuwa uwezo wa chuo kikuu kufanya utafiti na kufanya umeongezeka.

Naye, Dkt. Mohamed Zahir, Mhadhiri wa MUHAS idara ya Micro Chemistry na Microbiology ambaye ni mnufaika wa mradi huo amewashukuru kamati iliyosoma mapendekezo yote yaliyoandaliwa na idara ya Chuo cha MUHAS.

"Mimi ni mmoja ya wanufaika wa fedha za kufanya tafiti kwahiyo malengo yangu yatatimia kwa kutengeneza miundombinu ili tuweze kuchukua damu kutoka mifumo ya uzazi na kutengeneza benki ya sampuli za seli na vinasaba ambavyo vitakuja kutusaidia au kuwatibu wagonjwa wa Selimundu."

Kwahiyo tunawashukuru SIDA na ubalozi wa Sweden kwa kutoa fedha ambazo zitanisaidia kama mwanasayansi kukua kama mwanasayansi na kufanya tafiti ambayo Tanzania inastahiki ili kuweza kuboresha miundombinu ya nchi." Amesema Dkt. Zahir

Pia amesema wanaweza kufanya tafiti ambazo zitakazo fanana na tafiti za nchi zinazoendelea na nchi tajiri.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS Profesa Aporinary Kamuhabwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maabara ya Biorepository na kituo cha ubunifu maeneo yote katika chuo cha MUHAS Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Profesa Eligius Lyamuya wa Microbiology na Immunoology kutoka MUHAS akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maabara ya Biorepository na kituo cha ubunifu maeneo yote katika chuo cha MUHAS Mloganzila jijini Dar es Salaam.Matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad