HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 25, 2023

WAFANYABIASHARA WAASWA KULINDA 'BRAND' ZA BIASHARA ZAO

 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akiwa na viongozi wa Brela wakikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Maonesho ya kwanza ya siku tano ya Huduma za Brela, yanayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
"HAKUNA kitu kinachouza zaidi ya Brand,(utambulisho wa bidhaa au biashara) unaweza ukawa unatengeneza bidhaa zako vizuri lakini kama hautambuliki popote pale bidhaa yako itakosa soko, namna bora ya kuongeza dhamani ya shughuli, bidhaa unayozalisha ni lazima kusajiliwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ili utambulike."

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albart Chalamila wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya kwanza ya siku tano ya Huduma za Brela, yanayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam Oktoba 25, 2023. Amesema jukumu kubwa kwa wafanya biashara, Wajasiriamali wadogo ni kulinda Brand zao.

Pia amewaomba Brela na Baraza la Ushindani (FCC), wawasaidie wafanyabiashara kulinda utambulisho wa wafanyabiashara (Brand) ili waweze kupata faida za biashara baada ya kujisajili ili sekta binafsi iweze kurasimishwa na wanachi waone umuhimu wa kurasimisha na kuwa na ulinzi wa Brand zao.

Amesema mkoa wa Dar es Salaam kuna wafanyabiashara wakubwa, wakati na Wadogo, wajibu walionao Serikali ni kuhakikisha kwamba Wafanyabiashara walio katika sekta ya uchumi wanakua na wanarasimishwa.

Pia amesema Brela iwafikie wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati ambao bado hawajarasimishwa ili waendelee kurasimishwa kwa kusajili biashara, Makampuni ili kuendelea kukuza sekta ya Uchumi wa mkoa wa Dar es Salaam na Taifa kwa Ujumla.

Pia amewasisitiza wawafanyabiashara, Wajasiriamali wanatumia maonesho hayo kuweza kufanikisha mahusiano na wadau mbalimbali na kuzifikia taasisi zote ambazo zinaweza kufanyakazi karibu na Brela.

"Maonesho ya siku hizi 5 yatumike kufanya tathmini ya kina, Wadau wanaitizama vipi Brela na wanamaoni gani juu ya Brela, wanadhani ni kitu gani kiboreshwe." Amesema DC Komba

Pia amewaomba Brela kuona Umuhimu wa kutoa huduma kimtandao ili kuondoa Vishoka, dhuluma na utapeli katika kusajili kampuni na biashara na kuondoa watu wa katikati ambao wamewafanya Watanzania waone kama gharama za kusajili kampuni au biashara ni kubwa.

Pia ametoa rai kwa Brela kuendelea kutoa elimu ya namna ambavyo wanaweza kupata huduma za Brela kimtandao ili waondokane na Vishoka na watu kati wanaosababisha usumbufu kwa wananchi.

"Tukiimarisha ulimwengu wa kidigitali tutawasaidia wananchi wengi zaidi." Amesisitiza

Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maonesho hayo yaliyoandaliwa na Brela ili kujua huduma zote zinazotolewa na Brela ili kuondokana na Vishoka, Watu kati, wajanja wachache wanaosababisha kuonekana kama Brela lazima utoe fedha nyingi ili usajiliwe.

Kwa Upande wa Wajasiliamali, Wafanyabiashara waliohudhuria katika Maonesho hayo yaliyoandaliwa na Brela wameishukuru Serikali kupitia Brela kuleta maonesho hayo ambayo yatawaunganisha na wafanyabiashara na Makampuni
mbalimbali ili kubadilishana uzoefu anamna ya kufanya biashara.
Mkurugenzi wa Leseni, Andrew Mkapa akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba alipotembelea banda la Brela wakati wa maonesho ya siku tano ya kwanza yaliyoandaliwa na Brela na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba akiwa na viongozi wa Brela wakitembelea mabanda ya wajasiliamali na wafanyabiashara mbalimbali katika Maonesho yaliyoandaliwa na Brela na yanafanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad