HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 25, 2023

MLAWA AKEMEA BAADHI YA WAZAZI WANAOWAFANYIA VITENDO VYA KIKATILI WATOTO WA KIKE

 Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi ,(CCM)Wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa amekemea tabia ya baadhi ya wazazi wilayani humo kuwanyanyapaa watoto wa kike na badala yake amewaasa kubadili mfumo wa malezi ili kuwapa watoto haki sawa.

Aidha amekemea wazazi wa kiume wenye tabia ya kuwaingilia kimapenzi watoto wao wa kike suala ambalo ni la kinyama.

Alitoa rai hiyo ,kwenye mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Lugoba iliyopo Halmashauri ya Chalinze.

Mlawa anawataka wazazi na walezi ,kuacha vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto na kusema Kama Jumuiya wanafuatilia masuala hayo na kuchukua hatua.

Vilevile Mlawa, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili yanayotakiwa kwa kuzingatia tamaduni za watanzania.

"Tumekuwa tukifuatilia na kuwachukulia hatua ,wapo wengine wameshtakiwa na kuhukumiwa kwenda jela kutokana na vitendo vya kufanya ukatili kwa watoto na kuwabaka tena wengine ni wazazi wenyewe wa kiume kufanya vitendo hivyo watoto wao wa kike"

Mlawa pia alitoa rai kwa wazazi kushirikiana na walimu ,kufuatilia mienendo ya watoto wao mashuleni ili kuinua taaluma zao.

Mlawa ambae pia ni ofisa Habari wa makampuni ya Subash Patel ambao ni walezi wa shule ya Sekondari Lugoba alieleza awali walijenga mabweni matatu kupunguza mimba kwa wanafunzi wa kike, sasa wanatarajia kujenga uzio katika shule hiyo ili kudhibiti utoro.

Awali mkuu wa shule ya Sekondari, Lugoba Abdallah Sakasa changamoto inayowakabili ni ukosefu wa uzio ambapo inasababisha utoro kwa wanafunzi.

Sakasa alitaja changamoto nyingine, uhaba wa vifaa vya maabara kwa ajili ya elimu ya vitendo kwenye masomo ya sayansi, maktaba pamoja na mabweni.

Aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuidhinisha fedha, milioni 167.3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba saba vya madarasa na matundu ya vyoo kumi.

Alieleza kwamba, kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo saba , watakuwa hawana changamoto ya madarasa shuleni hapo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad