HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2023

TWCC YAPELEKA WANAWAKE 95 CHINA KUJIFUNZA VIWANDA NA BIASHARA

 

Mwenyekiti Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mercy Silla akizungumza leo Oktoba 14, 2023 na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha maandalizi ya Safari ya kwenda nchini China.
Matukio Mbalimbali.

CHAMA Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) chapeleka Wanawake Wafanyabiashara 95 Nchini China kujifunza masuala ya Viwada na Biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 14, 2023 wakati wa Kikao cha maandalizi ya Safari, Mwenyekiti TWCC, Mercy Silla amesema safari ya mwaka huu ni tano ikiwa ni mfululizo wa Safari za Mafunzo kwa Wanawake wafanyabiashara wa hapa nchini kutembelea China.

"Safari ya Wafanyabiashara ya kwenda China , tunaenda kwajili ya kuangalia kuona, kushiriki katika maonesho makubwa ya Canton Fair, ambayo tumeona ni vyema wafanyabiashara hapa nchini nao wakashiriki" Amesema Mercy

Lengo la Safari hiyo wwafanyabiashara na wanawake kwenda kuangalia fursa zilizopo za kimataifa, kuangalia mashine za viwanda, Vipodozi na dawa, Nguo, mashine za kilimo, mashine za kutengeneza Chakula, Mashine za kuongeza dhamani za malighafi hapa nchini.

Washiriki hao watajionea wenyewe, watajifunza, pia watakuwa na mikutano na watu wa Viwanda na watu wanaosambaza bidhaa mbalimbali wanazozihitaji katika biashara zao.

"Kwa shuhuda za waliowahi kwenda kujifunza nje wameona faida yake, wameweza kukuza biashara zao na Wameweka kuongeza kipato chao na wengine wanaenda kwa mara nyingine kwenda kununua mashine mbalimbali kwaajili ya kuja kuendeleza biashara zao hapa nchini." Amesema Mercy

Amesema Safari hiyo itachangia uchumi wa nchi yetu kwa sababu wao ni wafanyabiashara wa kati na wadogo ambapo ushiriki wao ni asilimia 54 ya uchumi wa nchi, pia amesema Safari hiyo inatambuliwa na serikali kwa kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara nchini.

Amesema Walishawahi kwenda Omani, Dubai na Uturuki kwaajili ya kujifunza biashara mbalimbali na kutembelea viwanda katika nchi hizo.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Uniform Point- Arusha, Witness Shoo amesema kuwa safari hiyo itamwezesha kwenda kuangalia mashine zitakazo mwezesha kuendelea kufanya kazi kwa urahusi zaidi hasa mashine zitakazo kuwa zinachakata taka masalia ya sweta na kutengeneza bidhaa nyingine ambayo ni mablanketi.

"Safari hii nimeamua kwenda mimi mwenyewe Nchini China kwenda kuonana mimi mwenyewe na wazalishaji, kutengeneza mahusiano ili muuzaji ajue anamuuzia nani ili nitakapokuwa nahitaji spea za mashine zitakapoharibika nijue nitazipata wapi moja kwa moja bila kupitia kwa mtu wapili ambapo ni kuongeza gharama." Amesema Witness

Pia amesema China ataenda kuangalia Mashine na vipuli vya gharama nafuu vya kutengeneza soksi kwaajili ya wanafunzi ambazo ukilinganisha na mashine aliyonayo kwa sasa.
Akizungumzia kuhusiana na fursa aliyoipata Mjasiliamali, Fransis Mlokozi amesema kuwa ni mara ya kwanza akupata fursa hiyo kupitia TWCC, ataenda kuangalia njia nafuu ya kupunguza gharama za ujenzi kwa kuangalia vifaa vya ujenzi ambavyo vitakuwa na gharama nafuu pia kuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara na wafanyabiashara wa China.

Pia amesema hapa nchini kunafursa ya kuchakata matunda ya msimu ambayo wakati wake huwa ni mengi na kuharibika.

"Kwahiyo katika Safari ya China katika Maonesho ya Canton Fair nitakutana na watu wanaotengeneza Mashine za kuchakata matunda na kukausha matunda yanapokuwa kwenye msimu ili msimu unapopita yaweze kutumika tena." Amesema Mlokozi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad