HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, October 7, 2023

TBS KANDA YA MASHARIKI YATEKETEZA VIPODOZI TANI NANE VYENYE VIAMBATA SUMU

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Mashariki limeteketeza tani nane ya bidhaa za vipodozi ambazo zilikamatwa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari hapo Jana Oktoba 6,2023 Mkuranga mkoani Pwani, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bw.Francis Mapunda amesema zoezi la kukamata bidhaa za vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku ni endelevu hivyo amewataka wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa hizo.

Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara wa vipodozi kufanya usajili wa vipodozi na kufuata orodha ya bidhaa za vipodozi ambavyo vimesajiliwa na kuruhusiwa kuuzwa.

Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanajiepusha na biashara ya bidhaa za vipodozi zenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku kuepusha usumbufu na gharama zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad