Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mikondo Miwili ya Uzalishaji Maji wa Kiwanda cha Suma JKT Bottling Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mikondo Miwili ya Uzalishaji Maji wa Kiwanda cha Suma JKT Bottling Jijini Dar es Salaam.
*****************
*CDF Mkunda ataka Suma JKT kubuni vyanzo mbalimbali vya kuingiza mapato
Na Chalila Kibuda, Dar es Salaam
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Jacob Mkunda amesema Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekuwa likitumika katika miradi yab mbalimbali hivyo lazima liendane na kasi hiyo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt.Samia Suluhu Hassan
Katika Miradi ya Sasa inayotekelezwa na JKT ni ujenzi wa Nyumba Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga pamoja na ulinzi wa bomba la Mafuta kutoka Hoima hadi Chongoleani Tanga.
"Tumepewa mradi wa kujenga nyumba 5000 Msomera Tanga,Kujenga Mjini mpya wa Dodoma na kusimamia ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi linalotoka Uganda hadi Tanga," amesema
Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa mitambo ya mikondo miwili ya uzalishaji maji ya kunywa yenye thamani zaidi Bilion Moja iliyofungwa kwenye kiwanda cha Suma JKT Bottling.
Amesema Shirika hilo bado linategemewa na serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye sekta mbalimbali huku akiwataka viongozi kuendelea kubuni miradi ya kimkakati na kuisimamia kwa weledi
Amesema kazi ya shirika hilo kubuni miradi ya kuzalisha kwa kutumia shirika la uzalishaji mali Suma JKT katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu huyo wakati wa uzinduzi huo wa kiwanda cha maji ameagiza Shirika la Uzalishaji Mali nchini,(Suma JKT) kukaa na wataalamu wake wa uchumi kutathimini kuangalia kujiendesha kwa hasara kwenye maji na kuja na mifumo ambayo haiwezi kupatikana na kubaki faida.
Amesema kuwa moja ya mfano kuongeza ukubwa wa chupa ambao utatumia maji yale yale na kizibo kile na wafanyakazi wale wale hivyo watakuwa wanajiendesha vizuri
Amesema shahuku yake ni kuona kiwanda hicho kinajiendesha kwa faida kwa kuzalisha bidhaa itakayoleta ushindani katika soko la maji nchini nkupata mapato badala ya kupata hasara.
"Shirika hili linaraslimali za kutosha ikiwemo wataalam wa uchumi mshauriane na kuja na mfumo mzuri wa uendeshaji utakaosaidia kiwanda kujiendesha na kupata faida zaidi,"alisema Jenerali Mkunda
"Ni muhimu kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya kujipatia fedha ili kulifanya shirika hili kuendelea kusimamia azma yake ya uzalishaji mali na kuwa msaada kwa nchini," amesema
Jenerali Mkunda amesema serikali bado ina imani kubwa na shirika hilo na jeshi la kujenga taifa kwa ujumla katika kuleta mageuzi ya kiuchumi ndiyo maana wamepewa dhamani ya kusimamia miradi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Uzalishaji mali wa Suma JKT,Kanal Petro Ngata amesema baada ya kupatikana kwa mitambo hiyo inaenda kuongeza ufanisi na uzalishaji wa bidhaa hiyo kwa wingi na kuleta ushindani sokoni.
"Mitambo yetu mipya inauwezo wa kuzalisha kuanzia milimita 350 hadi 650 na pia inauwezo wa kuzalisha chupa 500 kwa saa moja," amesema
Amesema wigo wa biashara unaenda kukua katika kuwafikia wateja wote tofauti na huko nyuma uzalishaji wake ulikuwa wa chini kutokana na ubora wa mitambo waliyokuwa wanatumia kuzalisha.
Amesema kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 2018 lengo likiwa ni kujiinua kiuchumi na kulifanya shirika hilo kujitegemea kiuchumi.
Amesema Mitambo hiyo yenye mikondo miwili imenunuliwa na kufungwa, ambapo mkondo wa kwanza una uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo 350 mls na 600 mls (kawaida na premier), lita 1 na lita 1.6. huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha chupa 10,000 kwa saa.
Amesema kwa Mkondo wa pili unazalisha maji makubwa yenye ujazo wa lita 13 na lita 18 pamoja na kuwa na uwezo wa kuzalisha chupa 500 kwa saa.
"Bidhaa hizi zimefanyiwa utafiti wa soko ili kukidhi matakwa ya wateja wetu Sambamba na ununuzi wa mtambo hii, Shirika lilifanya ukarabati wa majengo, kuboresha maabara, miundombinu ya umeme na ununuzi wa magari mawili (3.5 Tones) ambapo vyote kwa pamoja vimegharimu kiasi cha TShs 1,839,495,507.75"amesema
Amesema azma ya Shirika ni kuhakikisha Kampuni na miradi yake mbalimbali inakua na kuongeza vyanzo vya mapato vitakayowezesha Shirika kutekeleza malengo yake kwa ufanisi zaidi.
Hata hivyo amesema uzinduzi wa bidhaa hizo mpya utaongeza wigo katika sekta ya Biashara na Huduma na kuongeza wateja, na kuliwezesja Shirika kupata faida zaidi.
"Nitoe wito kwa Wakuu wa Kamandi, Vikosi, Shule, Vyuo pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutumia maji haya ya Uhuru Peak, kwani yana viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa"amesema
Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Hassan Mabena akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Ofisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele
amesema kiwanda hicho cha Maji ya Kunywa SUMAJKT Bottling Co Ltd kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na uwezo mdogo kiuzalishaji.
Amesema Hali hiyo ilipelekea Shirika kuweka mipango ya kuongeza Mikondo ya Uzalishaji ili kukidhi matakwa ya wateja wetu.
"Menejimenti ya Shirika chini ya Bodi ya Ushauri ilipitisha mapendekezo ya maboresho na hatimaye kuagiza mitambo itakayowezesha kuzalisha bidhaa mpya za maji ambayo ikikupendeza utaizindua leo hii"amesema
Aliongeza kuwa Shirika linaendelea kutekeleza Mpango Mkakati wake wenye lengo la kuongeza mapato na faida kuchumi na kijamii kwa kuboresha viwanda vilivyopo na kuanzisha viwanda vipya, ambavyo ni sehemu ya mipango ya Shirika.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akiangalia ubora wa maji yenye muonekano mpya mara baada Uzinduzi wa Mikondo Miwili ya Uzalishaji Maji wa Kiwanda cha Suma JKT Bottling Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment