*Dkt.Doriye aahidi neema nyingine miaka 60 ijayo
* Yanga waungana maadhisho ya miaka 60 ya NIC Insurance
NIC Insurance katika kutimiza miaka 60 imesema imeahidi kuendelea kuboresha huduma kwa wateja kwa kisasa zaidi kwa kuja Akili Bandia (Artificial Intellence) katika kuhudumia wateja
NIC Insurance itahakikisha inaendelea kuboresha huduma zake kwa kubuni huduma mpya lakini kushirikiana zaidi na jamii ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mmoja kwa mifumo rahisi ya kidijitali.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mendaji wa NIC Insurance Dkt. Elirehema Doliye wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kilichowakutanisha na watendaji wa wakuu wa timu ya yanga na wachezaji jijjnj Dar es Salaam.
Amesema maadhimisho ya miaka 60 ya shirika hilo yamekua ya manufaa makubwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kuliinua na kuliendeleza NIC Insurance ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Bima.
"Tunaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa shirika hili ambapo tunajivunia mafanikio makubwa ambayo tumeyapata kwa kipindi chote lakini pia tumekuja na mikakati itakayosaidia katika kuandaa miaka mingine 60 ijayo"amesema Doriye.
Amesema moja ya vipaumbele ambavyo wameviweka ni kuhakikisha wanawekeza kwenye TEHAMA kwa kuwa wabunifu zaidi kwa kubuni huduma ambazo zitabaki kwenye mioyo ya wateja kwani itakuwa kampuni ya kwanza ya kutumia akili bandia katika utendaji wake.
Amesema wataendelea kukuza biashara ndogo ndogo kwa kwa kupanua wigo wa kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Doriye ameongeza kuwa kuunga mkono vipaumbele vya serikali ikiwemo katika sekta ya kilimo kwa kutoa Bima ya kilimo.
Sambamba na hayo Dkt. Doriye amesema kuwa wataendelea kuwa karibu na jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo katika sekta ya Afya na mazingira.
"Hii ni Bima ya wananchi na tupo kwenye maazimisho ya miaka 60 lakini pia kuandaa miaka 60 ijayo tumejidhatiti kutoa elimu kwa wananchi lakini kushirikiana na wananchi hivyo tutakua na mabonanza mbalimbali ya michezo yatakayohusisha sekta binafsi na serikali wakiwemo waandishi wa habari"ameongeza Doriye.
Dkt.Doriye wanatarajia pia kufanya mazungumzo ya kitaaluma ili kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kuandaa video yenye historia ya Bima.
Aidha Dkt. Doriye ameongeza kuwa yote watakayoyafanya kama maadhimisho ya miaka 60 watashirikiana na timu ya mpira wa miguu ya Yanga.
Nae,Afisa Mtendaji Mkuu wa wa klabu ya yanga Andre Mtine ameishukuru NIC Insurance na kuhaidi kushirikiana nao katika kuhakikisha elimu ya Bima inamfikia kila mtu lakini pia kushirikia katika shughuli za kijamii ikiwa kama sehemu ya kutoa elimu.
"Sisi kama Yanga tunafurahia kuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya NIC Insurance kwani hii ni taasisi ya kwanza ya Bima na inafanya vizuri sana sisi tunaahidi kushirikiana nao"amesema Mtine.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Dkt.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwake jijini Dar es Salaam.
Mkurugunzi wa Masoko na Uhusiano wa NIC Insurance Karim Meshack akitoa maelezo kuhusiana taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Elirehema Doriye jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Timu ya Yanga Andre Matine akizungumza kuhusiana na Yanga kushiriki katika maadhimisho ya NIC Insurance , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance akimulisha Keki Afisa Mtendaji Mkuu wa Timu ya Yanga Andre Matine ikiwa ni kutimiza miaka 60 ya NIC Insurance.
Picha za matukio katika picha katika maadhimisho ya NIC Insurance.
No comments:
Post a Comment