HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 1, 2023

SERIKALI YAAGIZA WAFANYABIASHARA WANAOFANYA VIZURI KULIPA KODI KUPEWA MOTISHA

 

Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakati wa kufunga wiki ya mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD), jijini Dar es Salaam,  Kushoto kwake ni Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Tabu Shaibu.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Fedha,Hamad Hassan Chande amemuagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Alphayo Kidata kuwatambua na kuwapa motisha wafanyabiashara wanaofanya vizuri katika ulipaji wa kodi ili waweze kupewa vyeti na zawadi mbalimbali.

Pia amewataka wafanyabishara hao kushirikiana na TRA kufuata miongozo na matumizi sahihi za mashine ya risiti za kielekroniki (EFD) ili waweze kuchangia kodi itakayosaidia kuleta maendeleo ya nchi ikiwemo kujenga hospitali.

Akizungumza kwenye bonanza lililoandaliwa na TRA wakati wa kilele cha wiki ya EFD, leo Septemba 30,2023 Chande amesema kamishna huyo anatakiwa kuwatambua na kuwapa motisha wafanyabiashara wakubwa,kati na wadogo wanaofanya vizuri kulipa kodi ili wapewe vyeti na zawadi mbalimbali.

Amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa wawajibike kulipa kodi kwa kuwa ni jambo la maendeleo hivyo watoe risiti kwa wale wanaouza na wanaonunua wadai risiti kwa kwa maendeleo ya nchi.

"Matumizi sahihi ya EFD katika biashara ni muhimu kusimamia ukusanyaji wa mapato na kufanikisha uwazi na nidhamu katika mifumo ya kifedha nchini ambapo mashine hiyo ni kiungo katika jitihada ya kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti upotevu wa mapato ya nchi kuhakikisha yanarekodiwa kwa usahihi" amesema Chande

Aidha amewaambia wafanyabiashara hao kuwa wanapaswa kuhakikisha wanafahamu wajibu wao katika kutumia mashine za EFD na kufuata sheria,miongozo inayohusiana na matumizi yake.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA,Kidata amesema ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi ili kuliendesha gurudumu la maendeleo kwa pamoja ikiwemo kujenga hospitali na barabara shughuli zinazohitaji rasilimali fedha.

"Ninawaomba watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kulipa kodi bila ya kusukumwa na tunachokiomba kwenu ni kodi sahihi na wala siyo kodi ya kubambika na pia tuwe na utamaduni wa kutunza kumbukumbu zetu za biashara ukiuza ule muhamala uingize kwenye mashine za EFD unasomeka kwetu na wewe unabaki kwako,”alisema Kidata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad