HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 10, 2023

NAIBU WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UGANDA

 

Na. Neema Mbuja - KAMPALA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 10, 2023 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda ili kupeana taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii yanayoendelea nchini. 

Akitoa tathmini ya masuala mbalimbali ya kiuchumi, Naibu Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais anataka kuona nchi ikipiga  hatua kiuchumi na kuwataka wafanyakazi kumsaidia Mheshimiwa Rais kutimiza azma hiyo. 

"Fanyeni kazi kwa uadilifu na Mheshimiwa Rais anathamini Sana mchango mnaoutoa kama ubalozi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza uchumi" Amesema Dkt Biteko.

Akitoa tathmini juu ya masuala ya Nishati hususani Kuhusu masuala ya umeme Mhe. Dkt. Biteko amesema miradi yote ya kimkakati iko kwenye hatua nzuri na kutolea mfano wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kuwa litaondoa  changamoto ya upungufu wa umeme na kuwezesha vituo vya kuzalisha umeme wa maji kufanya matengenezo na kuongeza pia kiwango cha gesi ili kufidia mapungufu yaliyopo

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi amewataka wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini  Uganda kuhakikisha wanatumia vema  fursa za kibiashara zilizopo nchini Uganda kwa manufaa ya nchi yetu na kuongeza ushirikiano wa kibiashara na wadau wote.

Amesema, takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2022 uwekezaji kwenye masuala ya biashara ulikuwa karibu shilingi bilioni 138  kutoka Tanzania pekee na kuwa nchi ya tatu kwa uwekezaji nchini Uganda.
Kikao hicho kimedhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Wizara ya Mambo ya Nje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad