HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 10, 2023

Muhimbili yapokea msaada wa VITIMWENDO 21 vya TZS. 5.7MIL

 

 


Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa viti mwendo 21 vyenye thamani ya TZS. 5.7Mil kutoka kampuni ya Stufit Afrika PVT. Ltd kwa lengo la kusaidia wagonjwa mbalimbali wanaokuja hospitalini hapo.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi ameshukuru kampuni hiyo kwa msaada huo ambao utasaidia wagonjwa wanaohitaji usaidizi kutoka sehemu moja hadi nyingine.

" Tunashukuru kampuni ya Stufit Afrika PVT. Ltd kwa kuguswa na kuona uhitaji huu kwa wagonjwa ambao wengi wao ni Watanzania wenzetu ambao wanapitia changamoto mbalimbali za afya, kwani uhitaji ni mkubwa kulingana na wagonjwa tunaowahudumia,” ameongeza Prof. Janabi




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad