HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 3, 2023

MKURUGENZI MTENDAJI WA AKIBA COMMERCIAL BANK PLC AZINDUA RASMI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Bw. Silvest Arumasi, amezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Arumasi amewashukuru wateja kwa kuichagua na kuiamini Benki ya Akiba katika kuwahudumia. Aidha, ameendelea kuwaahidi na kuwahakikishia wateja huduma bora kutoka ACB.

Sherehe za huduma kwa wateja zina adhimishwa katika matawi yote ya ACB na hivyo, Bw. Arumasi amewaalika wateja wote kutembelea matawi ya Akiba kwa ajili ya kusherekea wiki hii ya huduma kwa wateja pamoja na kupata taarifa mbali mbali za huduma mpya na maboresho mbali mbali.

Pia, Mkurugenzi amewashukuru wateja wote walioshiriki katika zoezi la utafiti wa viwango vya uridhikaji katika utoa huduma yaani (Customer Satisfaction Survey) lililoratibiwa na kampuni huru ya kujitegemea kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uhuru wa kutoa maoni kwa wateja.

ACB ina utamaduni wa kufanya utafiti huo kila mwaka na hivyo amewasihi wateja kushiriki tena kikamilifu kwa lengo la kupata maoni na mirejesho itakayosaidioa kuboresha huduma zitolewazo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad