HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 3, 2023

MBUNGE KOKA AWAKOMBOA WAZEE VISIGA KWA KUWAPATIA ENEO LA UJENZI WA KITUO

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Baàdhi ya wazee katika kata ya Visiga iliyopo halmashauri ya mji Kibaha mkoani Pwani wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuwa karibu nao na kuwajali kwa hali na mali katika kusikiliza changamoto zao mbali mbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Wazee hao wametoa pongezi hizo wakati wa halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwakabidhi kadi zao rasmi zaidi ya 300 ambazo watazitumia katika kupata matibabu kwa urahisi pindi wanapoumwa ili kuondoka na na usumbufu ambao waliokuwa wanaupata.

Walibainisha kwamba kitendo cha Mhe.Mbunge wao kwa kuwaahidi kuwasaidia kwa hali na mali ikiwemo katika suala zima la huduma ya afya litakuwa ni msaada mkubwa kwa upañde wao.

Kadhalika wazee hao waliongeza kwamba wana Imani kubwa na Mbunge Koka ataweza kuleta mabadiliko mbali mbali kutokana na msaada wake wa kutoa eneo la kiwanja kwa gharama zake ili liweze kutumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuwasaidia wazee.

"Kwa kweli sisi Kama wazee leo tumefarijika sana kupata fursa ya kupatiwa kadi zetu ambazo kiukweli zitaweza kutusaidia katika kupata matibabu kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa kipindi cha nyuma na pia tunashukuru shirika la Videa ambao wamewezesha upatikanaji wa kadi hizi bila kumsahau Mbunge kwa kutoa kiwanja"walisema.

Kwa upañde wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alisema kwamba kwa kuwa lengo lake kubwa ni kuboresha sekta ya afya ameamua kuwatafutia eneo la kiwanja kwa lengo la kujenga kituo cha kudumu kwa ajili ya kuwasaidia wazee kupata huduma mbali mbali hususan za matibabu na mambo mengine.

Mhe.Koka alifafanua kuwa wazee ni watu muhimu sana katika jamii hivyo wanapaswa kuwekewa mazingira bora na rafiki ikiwemo kuwajali kwa kuwapatia vifaa tiba ambavyo vitaweza kuwa ni mkombozi katika matibabu pamoja na mahitaji mengine ya msingi.
"Nimeisikiliza risala yenu na kikubwa ili Jambo nimelichukua kwa mikono miwili na kikubwa kwa kuwa na mimi nina marafiki zao nina imani baadhi ya vitu wataweza kutusaidia kwa kushirikiana na ofisi yangu lengo ni kuwasaidia wazee wetu kwani na sisi lazima tutakuwa wazee ili alikwepeki,"alisema Mhe.Koka.

Mbunge huyo aliongeza kuwa katika kufanikisha azma ya shirika hilo la Videa pia atashirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo wa ndani na nje ya nchi ili mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha kudumu uweze kutimia na kuleta mabadiliko chanya kwa wazee hasa katika kuwatimizia mahitaji yao mbali mbali.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Videa Social Service Organization Tumaini Msheika alisema kwa sasa kituo hicho kinaendesha kazi zake za kuwahudumia wananchi katika majengo ya kupanga hivyo msada wa kiwanja walioupata kutoka kwa Mbunge Koka kwa ajili ya ujenzi utakuwa mkombozi mkubwa.

Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Kibaha mjini mwalimu Mwajuma Nyamka alisema juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya ni utekelezaji wa ilani hivyo hivyo ana Imani wazee hao wataendelea kusikilizwa na kupata matibabu kwa upendeleo maalumu kwani ni haki yao.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad