HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 17, 2023

JESHI LA POLISI LASEMA MAHUSIANO MAZURI KATI YAKE NA VYOMBO VYA HABARI YATABORESHA AMANI YA NCHI

 

JESHI la Polisi limesema mahusiano mazuri kati ya yake na vyombo vya habari yataendeleza umoja na amani nchini ikiwemo mahusiano mema na jamii.

Aidha limesema lipo kwenye mabadiriko ya kifikra na kufanya vyombo hivyo viwili kuwa na ushirikiano wa karibu katika kutimiza majukumu yao kwani uhusiano kati ya jeshi la polisi na vyombo vya habari hauwezi kuepukika kwa kuwa vinategemeana.

Kamishna Mwandamizi na Msemaji wa jeshi la Polisi nchini, (SACP), David Misime ameyasema hayo leo Oktoba 17, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mada kwenye mdahalo kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya jeshi hilo na waandishi wa habari.

Mdahalo huo uliandaliwa na Taasisi ya International Media Support (IMS) pamoja na umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa uratibu wa DCPC.

"Nchi itaendelea kuwa na amani na utulivu ikiwa kuna mahusiano mazuri kati ya Polisi na vyombo vya habari, waandishi wa habari na Jeshi la Polisi tunatakiwa tuitangaze nchi yetu vizuri kwa kuwa na mahusiano mazuri na kila pande iheshimu kazi za mwenzake",amesema Misime.

Amesema, jeshi la polisi lipo na falsafa ya kutumia Polisi Jamii, kwa lengo la kutambua mchango na kumshirikisha kila mmoja atambue nafasi yake katika Tanzania kuhakikisha nchi yake inadumisha ulinzi, usalama na mahusiano.

"Ili falsafa hiyii iweze kufanyakazi vizuri, ni lazima jeshi hili lishirikine na vyombo vya habari kwakuwa vina mchango mkubwa na mahusiano ya moja kwa moja na jamii kupitia taaluma zao.

Jeshi la polisi linahitaji zaidi vyombo vya habari na limekuwa karibu na vyombo hivyo husa pale linapotokea suala la taharuki ambapo wamekuwa wakifikisha taarifa kipitia media.

SACP Misime amesema, katika kuhakikisha mahusiano mazuri baina ya vyombo hivyo, teyari jeshi la polisi limeshaanza elimu ya utayari kwa askari wake katika kuelekea uchaguzi wa Serikali ya Mtaa mwaka kesho na ule uchaguzi Mkuu 2025 kwa lengo la kuondoa mitafaruku ambayo huwa hutolea kipindi hicho.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya amesema mdahalo huo utasaidia kuondoa changamoto katika vyombo hivyo viwili ambavyo nyakati zingine vimekuwa vikisigana katika kutimiza majukumu yao.

"Mahali kokote ambapo kunakuwa na kutoelewana kunakuwa na uwezekano mzuri wa kuelewana na kupata kesho iliyo bora ndani ya nchi yetu",alisema Simbaya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema waandishi wa habari na polisi wote wanafanya kazi za kijamii hivyo kuna umuhimu wa kushirikiana na kuleta usawa ambao utasaidia kuleta maelewano mazuri na kufanya nchi kuwa na twasira nzuri kwa nchi zingine.

"Waandishi zingatieni sheria, haki na wajibu ni muhimu sana, mahusianio yanapotea kati ya taasisi hizi mbili polisi na media/waandishi ni kutokana na kutojua haki zao.

Mfano kutojua haki na wajibu wa msingi katika kuzingatia maadili ya kazi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad