HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 15, 2023

Bayport yatoa msaada wa kompyuta 30 kuboresha elimu katika Wilaya ya Mwanga.





*Kutumia Tsh 40 Milioni Kuboresha Elimu katika Wilaya ya Mwanga




Taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania imetoa msaada wa wa kompyuta 30 kwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya mkakati wake wa Utawala wa Kijamii na Mazingira (ESG) kuboresha elimu katika shule za Tanzania ukiweka msisitizo mkubwa katika kuthamini elimu kupitia teknolojia.

Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule za sekondari za Kighare na Kamwala za Mwanga mkoani humo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport, Bwana John Mbaga alisema katika hafla hiyo wilayani humo jana kuwa, Bayport inaamini kila mtoto anastahili kupata elimu bora, kwani elimu na teknolojia zina jukumu muhimu katika kuwezesha hilo.

"Kupitia jitihada zetu za ESG, tumedhamiria kuziba pengo la miundombinu katika shule nchini Tanzania na kuwawezesha kizazi kijacho kwa zana zinazohitaji katika mafanikio yao."

Katika jitihada hii, Bayport imeungana na Airtel Tanzania na Taasisi ya Elimu ya Tanzania na kupitia ushirikiano huu, Airtel itatoa huduma ya intaneti bure, wakati Taasisi ya Elimu ya Tanzania itasambaza moduli ya kujifunza kwa njia ya kidigitali.

Upande wake, Bwana Christian Mtavanga, Msimamizi Mkuu wa Mfumo katika Taasisi ya Elimu ya Tanzania, alisema kwamba aina hii ya moduli inajumuisha masomo mbalimbali na mitihani ya iliyopita inayopatikana mtandaoni, kuhakikisha uzoefu wa kujifunza bila vikwazo kwa wanafunzi.

Kwa kuongeza, Afisa Mwedeshaji Mkuu wa Bayport, Bwana Nderingo Materu, alisema, "Ushirikiano huu unadhihirisha nguvu ya ushirikiano sekta binafsi katika kuleta matokeo chanya katika elimu. Bayport imetoa kompyuta 30, viti na meza 30, spika, na televisheni ya inchi 65 yenye thamani ya Tsh 40 milioni.

"Kwa kuunganisha rasilimali na utaalamu, Bayport Financial Services na washirika wake wanajenga mazingira ambapo kujifunza kwa kutumia teknolojia kunaweza kustawi," alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Bayport.

Tukio hilo lilihudhuriwa na wawakilishi kutoka Bayport, Balozi wa Bayport, Bwana Haji Manara, Taasisi ya Elimu ya Tanzania, na uongozi wa shule za Kamwala na Kighare.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bayport, Bwana John Mbaga (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada wa kompyuta 30 kwa Diwani wa Kata ya Kighare, Bwana. Bwana Innocent Mshemo, zilizotolewa na kampuni hiyo kama sehemu ya mkakati wake wa Utawala wa Kijamii na Mazingira (ESG) kuboresha elimu katika shule za Tanzania. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika shule za sekondari za Kighare na Kamwala za Mwanga, mkoani Kilimanjaro jana

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad