HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 20, 2023

Serikali yaingia makubaliano katika kusomesha Walimu wa kutambulika kwa viwango vya Kimataifa

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeingia makubaliano na Shirika la GF International kwa ajili ya kupeleka walimu wa vyuo vya ufundi kwenda kusoma nje kwa ajili ya ujuzi wa zaidi na kupata vyeti vinavyotambulika Kimataifa.

Makubaliano hayo kwa serikali kuwa na watalaam hao watapata vyeti vya kimataifa na kuweza kufanya kazi nchi yeyote.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo kwa niaba ya Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia , Mkurugenzi wa Ufundi na  Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara hiyo Dkt.Noel Mbonde amesema kuwa katika makubaliano hayo wameanza na wakufunzi wa Wanne wa Uundaji Vyuma wataokwenda Kusoma Nchini Marekani na Afrika Kusini na kwa miezi tisa na mzunguko wake ni walimu 12.

Amesema kuwa changamoto iliyokuwepo ni kuwepo kwa miradi inafanyika nchini hata mafundi wanashindwa kushiriki kutokana na kukosa sifa za vyeti vinavyotambulika kimataifa.

Dkt.Mbonde amesema walimu wataokwenda wakirudi watafundisha wanafunzi kuwa ujuzi wa ziada katika fani walizosomea.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imeweka mikakati ya elimu inayokwenda na ujuzi zaidi kuliko nadharia ili kupata wataalam wanaoweza kufanya kazi ya ziada kwenye fani zao.

Aidha amesema kuwa serikali ya awamu ya sita kutokana na jitihada za Rais kuna miradi mingi inakuja hivyo watanzania wanatakiwa kuandaliwa kwa kuwa na ujuzi unaotambulika kimataifa.

Mwasisi wa GF Foundation Michael Vallez amesema kuwa wataonufaika watambulika kimataifa na faidi nyingine watakuwa walimu wenye ujuzi wa ziada wa kufundisha wengine.

Mkufunzi wa uchomeleaji kutoka Mbeya Patrick Ngailo amesema kuwa atakwenda kupata mafunzo.nchini Afrika Kusini ambapo itakuwa ni faida kwa nchi na kushukuru serikali kuona mbali ya kuendeleza watu katika ujuzi bobevu

Matukio ya picha za pamoja katika makundi mara baada ya kusaini Makubaliano kati ya Serikali na Shirika la GFP Kutoka Marekani kwa ajili ya Kusoma Walimu nje ya nchi kupata vyeti vya Kutambulika Viwango vya Kimaitaifa.

Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Noel Mbonde na Mwasisi wa Shirika la GFP kutoka Marekani Michael Vallez wakibadilishana hati za  makubaliano   kati ya Serikali na Shirika la GFP kwa ajili ya kisoma elimu ya ujuzi wenye kutambulika katika viwango vya Kimataifa, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa  Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Noel Mbonde na Mwasisi wa Shirika la GFP kutoka Marekani Michael Vallez wakitiliana makubaliano   kati ya Serikali na Shirika la GFP kwa ajili ya kisoma elimu ya ujuzi wenye kutambulika katika viwango vya Kimataifa, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Ufundi na  Mafunzo ya Ufundi Stadi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Noel Mbonde akizungumza mara baada ya kutiliana makubaliano kati ya Serikali na Shirika la GFP kwa ajili ya kisoma elimu ya ujuzi wenye kutambulika katika viwango vya Kimataifa, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad