HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 25, 2023

BENKI YA NMB YAFURAHIA CMSA KUIDHINISHA HATIFUNGANI YA THAMANI YA SH.TRILIONI MOJA

 

 


OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema benki hiyo inayofuraha kupata idhini ya kutangaza programu yao ya Hatifungani ya Jamii ya miaka 10 ambayo thamani yake ni Sh.trilioni moja na kufungua dirisha la uwekezaji wa toleo la kwanza la hatifungani ya NMB Jamii Bond.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa hatifungani hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam Zaipuna amefafanua hatifungani ya NMB Jamii Bond itakuwa ni ya miaka mitatu itakayo dumu hadi Novemba 2026.

Ameongeza wawekezaji kwenye hatifungani hiyo watajipatia riba ya asilimia asilimia 9.5 kwa mwaka, inayolipwa mara nne kwa mwaka.

"Kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hii ni Sh.500,000 na inaweza kununuliwa kwa kujaza fomu zinazopatikana kwenye matawi yote ya Benki ya NMB, au mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam waliopewa leseni na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

"Dirisha la uwekezaji la hatifungani hii ya NMB Jamii Bond lipo wazi kuanzia sasa hivi na mwisho wa kupokea maombi ya ununuzi ni Ijumaa 27 Oktoba 2023 saa kumi na moja jioni."

Ameeleza baada ya hapo hatifungani hiyo itaorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuwapa fursa wale ambao hawakuwekeza kwa wakati iko wazi kwa umma, wakimaanisha zinaweza kununuliwa na watu binafsi, makampuni na pia taasisi.

"Tumeweka malengo ya kukusanya Sh. Bilioni 75, huku Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ikiruhusu ongezeko la mpaka Sh. bilioni 25."

Kuhusu Toleo hilo la Kwanza amesema Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeidhinisha uuzaji wa hatifungani ya dola za kimarekani million 10 ikiruhusu ongezeko la mpaka dola za kimarekani milioni tano na kufanya kuwa na dola milioni 15, itakayouzwa kwa mashirika na wawekezaji walioko nje ya Tanzania.

Zaipuna amesema hatifungani ya Jamii ambayo imezinduliwa inalenga kukusanya fedha ambazo zitatuwezesha kutoa mikopo inayolenga kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Ametoa mfano wa mikopo hiyo ni mikopo kwa ajili ya miradi ya nishati mbadala, kuzuia na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, usimamizi wa maji na maji taka, usafiri safi, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Pia kuwapa nguvu wanawake na usawa wa kijinsia, nyumba za bei nafuu, usalama wa chakula, huduma muhimu (afya na elimu), na Vijana.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wote waliowaunga mkono na kusaidia hatifungani hiyo kuingia sokoni. "Naomba kulishukuru shirika la Financial Sector Deepening Africa (FSD Africa) kwa kuileta hatifungani hii katika soko.

"NMB tumefanya kazi na FSD Africa ambao walitoa mchango mkubwa wa Kitaalam katika mfumo wa hatifungani hii. Vilevile tulipata msaada wa Kitalaam kwa ajili ya maoni ya upande wa pili (yaani Second party Opinion) kutoka kampuni ya Sustainalytics.

"Niwashukuru Bodi na Uongozi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Bodi na Uongozi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Benki Kuu ya Tanzania, Mshauri mwenza ABSA Bank Tanzania Limited alieshirikiana na wataalamu wetu ndani ya Benki ya NMB."

Wengine ambao amewashukuru ni Mshauri wa Sheria, Rex Attorneys, Mtoa Taarifa za Mahesabu, KPMG na Dalali mdhamini, Orbit Securities Limited pamoja na Msajili wa Hazina.
Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kulia) wakizindua kwa pamoja Hati Fungani ya Jamii ya NMB 'NMB Jamii Bond' jijini Dar es Salaam leo Septemba 25, 2023.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto), akipokea Waraka wa Matarajio ya Programu ya Utoaji wa Hati Fungani ya Muda wa Kati (MTN) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, wakati wa uzinduzi wa NMB Jamii Bond.








Wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad